Wanawake wa siku hizi bana!

adakiss23

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
4,732
Reaction score
4,901
Yaani mnamkuta mdada.. Asubuhi akiamka yuko Bar anakula supu mchana Bar tena chips jioni yuko ktk pedicure n manicure anajiandaa na mtoko. Usiku ukiingia yuko Bar tena nyama choma na bia. Sasa unajiuliza hivi huyu anapika saa ngapi? Anafanya usafi saa ngapi? Ukimuoa mdada kama huyu si unajiandalia ugonjwa wa moyo? Je ataleaje watoto? Au ndo walewale anamnyonyesha wiki 1 then maziwa ya kopo yanahusika. Ndo wonda mitoto ya siku hizi vichwa maji cz tangu tumboni keshakunywa bia viroba konyagi maziwa ya kopo ya kutosha. Badilikeni dadazangu! Othawize mtamegwa sana na minjemba.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hapa anataka kusema kuwa angalau awe anapika
 
unataka single ladies wakae nyumbani wafanye nini?? enjoy life while you can, hayo ya watoto yatakuja after 10 pm
 
Ngoja waje . . . . . . . . !!
 
Punguza munkari kaka, duh! habari za huko uliko kwanza?
 
Ushachakachuliwa jomba?!mbona unalia hivo?!
 
Wote mnaotoa povu kuna wezekano jamaa kawagusa kinamna...!!!!!!poleni bana, nenepeni sanaa muwe na matumbo makubwa na mavitambi ka mlima, maana mmeona cha kuiga ni misupu na kunywa bia zisizo na staha..
 
Give me a breaaaaaaaaak! We ushaona huyo dada bado hajapata mwenza, sasa hizo ni katika promo, biahsara ni matangazoo! Ohooo! Unataka ashinde na mkaa jikoni afu nani amuone? Muuza mkaa au samaki? Aaaaah! Mwache mwenzio aende sehemu kwenye inteterlect minds apate nae interlectual wake! Samaki havuliwi shambani katuuu! Hizo manicure muhimu, we mkeo kakomaa mikono kwa kufua nepi na kodrai zako, utataka nyumba ndogo mikono lainiii!
 
ningeweza kumuelewa mwandish kama angeniambia ni watu wa aina gani ambao yeye anawaongelea. kama bidada hiyo ni hobi yake unataka ake numban kufanya nini? kuna watu hobi zao ni kwenda bar for a drink na kupiga story kuna wengine hobi ni kwena na hubbys maeneo yao kula bata sasa sijui wewe unasema haya kivipi.

mwanamke anajipamba na lazima aende salun swala la kunyonyesha nalo linaegemea kuna wengine wananyonyesha hata mika 3 lkn kwenye vitivirefu huwakosi inategemea tu ameschedule vip ratiba yake. manake anakamua maziwa anayaacha kwa ajili ya mtt.

haya ambao ni singles that is their time sijui kwanini unaumia sana ukawasahau vijana wanaoshinda wakicheza pool table siku nzima kijiwen huku wakigida mvinyo na manyama.
 
Badilikeni dadazangu! Othawize mtamegwa sana na minjemba.

Sijaelewa uhusiano wa hii sentenso na suala la kumegwa.
BAK, naomba unisaidie kumuwekea huyu ndugu ile wimbo ya Nyoshi El sadaat 'Sio kila mwanamke aendae bar ni malaya'
Natanguliza shukrani.
 
Last edited by a moderator:
Haahahahahahahahahahahaaha
da umenikumbusha dada mmoja anaitwa Natalia



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…