Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
VIJANA wa kike wameshauriwa kujiunga na masomo ya ubaharia, ili kuziba pengo la uhaba wa jinsi ya kike katika sekta ya Uchukuzi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati akihitimisha maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani leo.
Amesema kwa mujibu wa takwimu za shirika la ubaharia la kimataifa (IMO), kuna zaidi ya mabaharia million 1.6 duniani, huku Tanzania ikiwa na mabaharia 9000 lakini wanawake ni pungufu ya asilimia moja.
"Mabaharia ni muhimu katika kukuza uchumi nchini ni nyenzo muhimu pia katika kulinda mazingira kwa kudhibiti utupwaji wa taka hatari katika maji zinazoweza kuleta madhara kwa viumbe vinavyoishi majini.
"Tuendelee kulinda mazingira yetu kwa kuepuka uvivu haramu na tujenga hali ya kujifunza ili kuyatunza," anaeleza Masala.