Wanawake wana haki ya kubaki na majina yao ya ukoo (surname) baada ya kuolewa

Wanawake wana haki ya kubaki na majina yao ya ukoo (surname) baada ya kuolewa

Willima

Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
26
Reaction score
39
Wanawake kubadili majina yao ya ukoo (surname) baada ya kuolewa na kufuata majina ya waume zao ina onyesha au kuashiria hali ya utegemezi wa mwanamke kwa waume zao, mwanamke kufuata jina la mume wake baada ya kuolewa kunaashiria kuwa yeye ni mali ya mwanaume (mume wake), na anakosa mamlaka ya kufanya maamuzi bila ruhusa ya mwanaume (mume) na pia kufanya kila anachoambiwa na mume wake kwakua yeye sasa amesha kuwa mali ya mume wake.

Na kwakuwa mwanamke anataka kutunza jina la mume wake yaani kubaki katika ndoa anafanya kile anacho amriwa na mume wake hatakama nikibaya na hakina faida kwakwe, na hata kuvumilia ukatili anao fanyiwa na mume wake.

Kwanini mwanamke asibaki na jina lake baada ya kuolewa?, Kwani kuna athari gani mwanamke asipo badilisha jina lake na kufuata jina la mwanaume (mume) baada ya kuolewa?, na je kuna athari na utofauti gani mwanamke akibadili na kufuata jina la mumewake bada ya kuolewa?.

Toa maoni yako juu ya mada hii.
 
Wakati utamaduni wa baadhi ya wanawake kubadilisha majina na kutumia ya familia za wenza wao, ukionekana kama njia mojawapo ya kukuza upendo, wanasheria wameonya kuhusu utamaduni huo na kueleza kuwa una athari nyingi ikilinganishwa na faida.

Baadhi ya wanasheria hao wameeleza kuwa kubadilisha jina kunaweza kumletea usumbufu mhusika, na wakati mwingine kuingia kwenye mvutano pindi ndoa inapokoma.

Kuna ushahidi wa matukio kadhaa ya wanawake kutakiwa kusitisha kutumia majina ya wenza wao, baada ya ndoa kuvunjika ilhali walishajitambulisha kwa majina hayo tena kisheria.

Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, wakili wa kujitegemea, Bashir Yakub alishauri kuwa ni vyema wanawake wakaachana na utaratibu wa kubadilisha majina, kwa kuwa faida zake ni chache ukilinganisha na hasara.

Kwa mujibu wa Yakub, faida pekee inayoonekana baada ya mke kutumia jina la mumewe ni kutimiza lengo la kuingia kwenye familia hiyo na kuwa mwili mmoja, lakini mambo huwa tofauti pale ndoa hiyo inapofika ukomo na wenza hao kulazimika kuachana.

Alisema mbali na usumbufu unaoweza kujitokeza baada ya ndoa kuvunjika, matumizi ya jina la ukoo mwingine yanaweza kuleta shida kwenye utambulisho.



Wakili huyo alifafanua kuna baadhi ya taasisi za Serikali zinazotoa nyaraka nyeti kama vile vyeti vya kuzaliwa au vyeti vya elimu ambazo huwa hazitakiwi kubadilisha jina, hivyo mhusika licha ya kubadilisha jina pia atatakiwa kuwa na nyaraka za jina alilosajiliwa awali.

“Binafsi nikiambiwa nishauri ningewashauri wanawake kuachana na huu utamaduni. Ukiangalia kwa kina hasara ni nyingi na hakuna uthibitisho wowote kwamba ukitumia jina la ukoo wa mumeo ndoa itakuwa imara zaidi.

“Ikitokea umetumia jina la ukoo wa mumeo kwenye biashara au utambulisho mwingine wowote na yeye akaamua jina hilo lisitumike baada ya ndoa hiyo kukoma, jambo hilo linaweza kukuyumbisha kwa namna moja au nyingine. Kesi hizi zipo na binafsi nimeshawahi kukutana nazo.

Kwa mfano, ilikuwepo moja ambayo nimeifanyia kazi; mume alisimama kidete hataki jina lake litumike kwenye biashara ya aliyekuwa mkewe,” alisema wakili Yakub na kuongeza;

“Hata ikitokea unafuatilia hati ya kusafiria, itakuchukua muda mrefu kujieleza ukilinganishwa na yule ambaye nyaraka zake zote zinaonyesha jina moja, hivyo kwa kifupi kuna changamoto.”

Hilo liliungwa mkono na mwanasheria mwingine ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake akieleza kuwa hasara za kubadilisha jina ni nyingi kuliko wengi wanavyofikiria.

Alisema inamfanya mwanamke kupoteza utambulisho wake uliokuwa ukifahamika awali, kitu ambacho ni muhimu katika harakati za kimaisha.

Pia, alisema kutumia jina la ukoo mwingine inaweza kumfanya mwanamke kunyanyasika, akionekana kama anapata hisani kwa kutumia jina hilo.

“Katika familia zetu za Kiafrika si kitu cha ajabu kusikia hakuna maelewano kati ya mke na mawifi, au mashemeji.

Sasa hawa wanaweza kuona huyu kutumia jina la ukoo wao ni fahari kwake, basi hapo ndipo unyanyasaji unapoanzia, huku wakihoji kwa nini utumie jina letu kwanza wewe sio wa kwetu,” alisema mwanasheria huyo.

Hata hivyo, wakili Yakub alibainisha kuwa katika miaka ya karibuni wanawake wachache wamekuwa wakibadili majina yao baada ya kufunga ndoa ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Sasa ni wanawake wachache wanaofanya hivyo, huenda ni kwa sababu ndoa zenyewe zimekuwa hazidumu au wameshaona athari za kubadili. Wapo wachache wanaoendelea ila wengi siku hizi wanatumia majina yao ya awali.”

Rhoda Otaigo mkazi wa Chang’ombe jijini Dar es Salaam, alisema licha ya kuolewa hatumii jina la ukoo wa mume wake kwa kuwa haoni sababu ya kufanya hivyo.

“Sioni kama kuna ulazima wa kubadilisha jina, nimeolewa na ninatambua kuwa yule ni mume wangu, lakini sioni ulazima wa kutumia jina lake.

Kwanza tayari natambulika kwa jina langu, pili siku hizi ndoa zenyewe hazieleweki ikitokea mmeachana inakuwa shida, yaani nianze tena kuingia kwenye kibarua kingine cha kubadilisha jina; hapana acha tu nibaki na jina langu,” alisema Rhoda.


Kauli ya mwanasaikolojia

Akizungumzia hilo, mwanasaikolojia Saldin Kimangale alisema wanawake wengi wanatumia majina ya ukoo wa wenza wao kwa ajili ya usalama na kuonyesha utambulisho.

“Huu ni utaratibu ambao jamii tumeutengeneza, ila sioni kama ni sahihi; unaweza kumsababishia mwanamke kupoteza haki zake na hata utambulisho wake, kwa kuwa anaamini kwamba anapata usalama au kuonekana ameolewa kwenye familia fulani,” alisema Kimangale.

Mshauri wa uhusiano, Deogratius Sukambi anasema mazingira ya sasa yamefanya wanawake kukosa umuhimu wa kutumia majina ya waume zao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
 
Una hoja ila Hapa umeleta madai ya siyo na msingi,

"Na kwakuwa mwanamke anataka kutunza jina la mume wake yaani kubaki katika ndoa anafanya kile anacho amriwa na mume wake hatakama nikibaya na hakina faida kwakwe, na hata kuvumilia ukatili anao fanyiwa na mume wake."

Yaani kisa jina ndio akubali kuteseka? Kila anaachosema mumewe asipinge!! Mzee unajua mwanamke ana haki zake ndani ya ndoa?

Hapo unazungumzia ndoa ipi, kuna za kimila, kiserikali, kidini(uislam, ukristo, budha, hindu etc,) wote hao wanaoana na kutoka dini moja kwenda nyingine ndoa inakuwa tofauti kisheria na kimaadili.
 
Sio lazima kubadili ila wengi wanaobadili hua wanafanya kwa mapenzi yao binafsi na si kwa hizo sababu ulizoziainisha hapo.
 
Unajua maana ya kuolewa lakini?

Unajua maana ya mtu kuitwa Mke?

Mwanamke akishaolewa anakuwa chini ya miliki ya Mume wake,
Yeye ndiye Baba yake, mume, Kaka, na kila kitu anakitegemea Kwa Mumewe Kama alivyokuwa kwao.

Kuolewa ni kukabidhi mamlaka ya mwanamke Kwa mwanaume. Kutawaliwa na Mume.

Hiyo ndio maana ya ndoa.

Hakuna USAWA baina ya mwanamke na Mwanaume pale wanapofunga ndoa. Mmoja huwa mkubwa/Mtawala ambaye ndiye mume, mwingine huwa mdogo/mtawaliwa huyu huwa Mke
 
Michelle Obama
Hilal Clinton
Ete
Etc

Hayo ni baadhi ya majina ya kutoka ubeberuni. Na hawa ndio sehemu ya machipuko ya demokrasia na haki binafsi za binadamu
 
Mnazunguka sana mbona mnakubali kulipiwa mahari huoni kwamba kulipiwa mahari mnauzwa kama bidhaa.

Nyie hamna tofauti na wazanzibar wanasema muunganono unawanyonya lakini hawataki kutoka
 
Huu
Mnazunguka sana mbona mnakubali kulipiwa mahari huoni kwamba kulipiwa mahari mnauzwa kama bidhaa.

Nyie hamna tofauti na wazanzibar wanasema muunganono unawanyonya lakini hawataki kutoka

Huu Muungano ni MTEGO wa Russia na Ukraine 😂😂😂
Mzee alizidiwa akili na Kijana...
 
hio tabia mnayo nyie watu msiokua na Mungu,Dini wala Mtume ila kwetu sisi huu upuuzi hakuna ...

faida yake labda mnaijua nyinyi wenyewe
 
Back
Top Bottom