kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Unapouliza mapungufu kwenye masuala ya demokrasia yetu nchini ni rahisi sana kusikia kuwa demokrasia yetu bado ni changa sana ukilinganisha Na nchi za marekani Na ulaya, hivyo bado tunajifunza polepole ili tufike kwa wenzetu wenye zaidi ya miaka 200 na kuombwa tusijilinganishe nao.
Uchanga huu wa miaka 60 unatumika kuhalisha mapungufu yaliyoko kwenye demokrasia Na maendeleo nchini. Hata hivyo kasi tuliyonayo kwenye haki za wanawake kwenye uongozi kuelekea 50/50 ni kubwa kuliko nchi ya Marekani, Uchina, India, Uarabuni Na Ulaya zenye zaidi ya miaka 200 ya kujitawala. Hadi leo Marekani haijawahi kuwa Na Rais mwanamke, hawajafikia 50/50 kwa wabunge Na mawaziri. Hapa kwetu tunataka kuaminishwa kuwa kwa miaka 60 wanawake walionewa sana na wanaume hivyo tumechelewa sana kufikia 50/50.
Hebu tufanye utafiti kutoka kwa wenzetu wenye zaidi ya miaka 200 ya Uhuru Na demokrasia ni kwanini wanawake sio 50/50 kwenye ofisi zote hadi Leo. Hii itatusaidia tusijekuharibu nchi yetu au kutengeneza shida ambayo itakuwa ngumu kuitatua huko mbeleni. Lazima majibu wanayo.
Kwanini kuna wakati tunaona miaka 60 ni michache lakini kwa wanawake tunaiona ni mingi mno?