Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
WATAWA WA MAPINDUZI - The
Revolutionary Nuns
Mabinti VIPANGA na WAZURI wa sura waliokua wakichaguliwa na GADAFFI mwenyewe. Licha ya UREMBO na AKILI nyingi, Mabinti hawa walikuwa wamepikwa KUUA. Kwa miongo 2 walijitoa KAFARA kumlinda MTAWALA mkongwe wa LIBYA.
Mwaka 1979, Kanal Muammar Gadaffi alifungua Chuo cha wanawake cha kijeshi cha Tripoli, chuo ambacho baadae miaka ya 80 kilizalisha mabinti wakakamavu waliopewa jukumu la kumlinda Kiongozi wa Libya. Alipoulizwa sababu ya kwanini ameamua kuchagua walinzi wa kike Gadaffi alijibu....
.kuwa sababu kuu ilikua ni Mama yake mzazi, Gadaffi alidai kuwa mama yake alikua askari wa upinde wa daraja la juu ndani ya kabila la Bedouin, hivyo aliwahi kumuahidi kuwa atafanya juu chini kuongeza ARI ya wanawake katika jeshi na nyanja mbalimbali za juu nchini Libya....
.Licha ya sababu alizotoa Gadaffi, inasemekana sababu kubwa ilikuwa ni mawazo ya Gadaffi kuwa ni vigumu kwa walenga shabaha wa kiarabu kuwaua wanawake. Watawa wa mapinduzi walipitia programu ya miaka mitatu ya mafunzo katika chuo cha wanawake cha kijeshi cha Tripoli....
wakiwa chuoni hapo walipewa mafunzo yote ya kijeshi, ikiwemo kulenga shabaha, kurusha makombora, mawasilianao, ngumi na karate. Waliofuzu mafunzo hayo makali walikula kiapo kulinda mapinduzi ya mwaka 1969 na kujitoa kumlinda kiongozi wa mapinduzi Kanal Gadaffi....
..waliofuzu walikuwa wanapita kwenye mchujo wa mwisho ambao ulikuwa ukifanywa na Gadaffi mwenyewe, na baada ya mchujo huu walikua wanakula kiapo cha mwisho cha utii, kiapo ambacho kilikua kinawazuia kufanya mapenzi na kuolewa na kuapa kujitoa kumlinda Gadaffi mpaka kifo....
.Walinzi hawa wamekuwa wakimlinda Gadaffi tangu miaka ya 80 mpaka kifo chake. Kwa kipindi chote cha huduma yao wamekua wakipitia changamoto za hapa na pale lakini kubwa ni ile ya mwaka 1998 ambapo msafara wa Gadaffi ulivamiwa na kukatokea mapigano ya kurushiana....
..risasi. Katika mapigano hayo Mlizi mmoja aliyejulikana kwa jina Aisha alipigwa shaba na kufa papo hapo wakati akiwa kwenye harakati za kumlinda Gadaffi, inasemekana Aisha alijiweka mbele ya Gadaffi baada ya moja ya wavamizi kutaka kumtungua hivyo risasi ikampata yeye...
katika mpambano huo alikufa Aisha peke yake na watawa wengine saba walijeruhiwa wakati Gadaffi alitoroshwa samala salimini. Kwenye moja ya mazungumzo ya televisheni aliyewahi kuwa askari wa kundi hilo Bibie Faita alikaririwa akisema kwamba....
"Bila Gaddafi, wanawake wa Libya hawatakuwa na maana tena, Ametupa maisha na niko tayari kufa kwa ajili yake. Ni BABA, KAKA na RAFIKI kwa taifa, hujui tu ni jinsi gani alivyo mnyenyekevu." Katika kipindi cha mwishoni cha utawala wa Gadaffi kuliibuka tetesi kwamba mabinti....
..hao wamekuwa wakibakwa na kunyanyaswa kingono na Gadaffi, vijana wake(watoto wake wa kiume) na baadhi ya viongozi wa kada za juu wa serikali ya Libya. Baadhi ya watawa hao waliwahi kusema wanaamrishwa kuua waasi wa ndani wa serikali vinginevyo wangeuawa wao...
...Mwaka 2011, baada ya kuibuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya, Gadaffi alikuwa salama kwenye kasri yake ila baada ya hali kuzidi kuwa mbaya alitoroshwa na kwenda kujificha kusikojulikana na watawa wake. Mwezi Agosti mwaka huo baada ya Kanali Gadaffi kukamatwa....
.kuuawa na mwili wake kuanikwa mitaani. Inasemekana baadhi ya watawa ambao walikua waaminifu kwake mpaka mwisho pia walikamatwa naye na kuteswa ikiwa ni pamoja na kufanyiwa unyama, kubakwa na baadae kuuawa kikatili na huo ukawa mwisho wa huduma yao na kikundi hicho.....
.The Revolutionary Nuns - Watawa wa Mapinduzi walikuwa kivutio kikubwa kwenye misafara ya KANAL MUAMMAR GADAFFI na wanabaki kwenye historia kama kikundi pekee ya walinzi wakike tupu wa kiongozi wa taifa.
'MWISHO