Wanawake wanamvuto mkubwa kwenye biashara wakibadilika wanatoboa kirahisi

Wanawake wanamvuto mkubwa kwenye biashara wakibadilika wanatoboa kirahisi

Wang Shu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
2,562
Reaction score
3,715
Enyiiiii! Wanawke tambua kuwa mnamvuto wa kipekee sana kwenye biashara,mnaweza kujikusanyia wateja wa rika mbalimbali na jinsia zote kama mkitaka na kujirekebisha tabia ya nyodo na dharau kwenye biashara.

Wadada wengi wakiwepo kwenye biashara,yake au amejialiwa atoe uduma basi nyodo na dharau zake zote za mtaani anazileta kwenye biashara

Wanawake wakiuza biashara ya mavazi ya kiume wanatupatia sana wanaume,kuna mdada ananiuzia viatu anatembeza mtaani,nimeshangaa jinsi alivyokariri rangi za nguo zangu

T-shirt na suruali zangu ata kama siivai mara nyingi, akipata kiatu kinachoenda na rangi ya T-shirt yangu lazima anitafute anishawishi ninunue na kunambia nikivaa na nguo flani nitapendeza sana na kweli siku nikivaa najiona kabisa kuwa uku sasa ndio kuvaa nakupendeza

Amekuwa maarufu sana mtaani na ameshafungua ofisi sasa ivi tunamfwata yeye kazi yake kutupigia simu wateja wake wa kudumu na kwenda kuchukua bidhaa.

Namuamini sana hajawai kunivalisha kitu kibaya wanawake ni waaminifu kwenye biashara akikuambia hiki kizuri ni kweli kizuri sio kama wazee wakuveshana.

Kuna mdada mwingine yeye anauza mishikaki,hakika amekuwa watofauti na nimekuwa mteja wake wakudumu ata kama sina pesa nimekuwa mteja mwaminifu kwake ananipatia mishikaki.

Anaitwa "Sister Mishikaki" jina la kazi ameshika vijiwe vyote vya wauza mishikaki hakika ameongeza kitu kwenye biashara yake amekuwa mbunifu kidogo anauza mishikaki ya nyama ng'ombe,ya kuku, na kitimoto kwaiyo ukifika kwake unachagua wewe unataka kula nini.

Ufanisi wa hali juu kijiwe bora cha mishikaki sijawai kuona wateja tunaweka foleni.

Zipo shughuli nyingi wakifanya wanawake kwa ufanisi mzuri ni rahisi kufanikiwa kwa sababu wanahuruma, upendo na kujali.

Sio wavumilivu kwa wateja, kupandwa na hasira haraka,dharau, nyodo bila kusahau na wivu wakirekebisha ivyo wanatoboa kirahisi saaaaana.
 
Ni scientific fact kua biashara yenye jina la kike au mhusika ni mwanamke hua inamfanya mteja ajihisi katika mikono salama.

Mfano Abdallah Cakes na Aisha Cakes utaingia wapi? Ukisemea kuhusu McDonalds unajua ile logo yake actually inamaanisha matiti?

Also in every general rule there is an exception so wadada wakichangamka odds are in their favour.
 
nitaingia Aisha Cakes 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Ni scientific fact kua biashara yenye jina la kike au mhusika ni mwanamke hua inamfanya mteja ajihisi katika mikono salama.

Mfano Abdallah Cakes na Aisha Cakes utaingia wapi? Ukisemea kuhusu McDonalds unajua ile logo yake actually inamaanisha matiti?

Also in every general rule there is an exception so wadada wakichangamka odds are in their favour.
Sielewanagi na jinsia ya KE kwenye mishe zangu!
Na mtoa huduma akiwa KE nakwepa kabisa hilo duka, n.k.
Wana customer care mbovu sana!
Wajue tu nanunua bidhaa/huduma, na kigezo ni customer care, si jinsia.
 
Back
Top Bottom