Kituko kipo facebook bwana. Mtu anakutumia friendship request hata humjui. Ukimuaccept, message ya kwanza anakusalimia. ya pili anakuita dear, ya tatu sweet, ya nne my love, ya tano matatizo yake, inayofuata anaomba hela. Hizi message zote unazipokea in the same day, pengine ni muda wa saa moja tu. Huwa najitahidi sana kujibu zile zote za awali, lakini akishaniambia anaomba hela, basi ndo mwisho wa kujibu message zake.
Au mwingine anafuata the same trend halafu anamalizia na kuomba namba ya simu kwa kisingizio cha eti ana jambo private anataka akushirikishe. Ukimpa tu you are gone, kila siku atakupigia kukueleza hili mara lile akitaka umsaidie hela.
Hivi najiuliza akina dada wa Tanzania hali zao zimekuwa mbaya kiasi hiki? Yaani mtu unamwona kama ni dada wa heshima kweli, lakini anakutongoza live na kukuomba hela as if mnafahamiana kwa muda mrefu. Halafu cha kushangaza wengine wameandika kwenye status zao kwamba ni married. Nafikiri hali ya nchi sasa imefika pabaya kwa kweli!