Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
WANAWAKE WANAWEZA, TANROADS YAHIMIZA HAKI, USAWA NA UWEZESHAJI KATIKA UHANDISI
Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Motta Kyando, ameonesha furaha yake kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika jijini Arusha. Maadhimisho hayo, yatakayofikia kilele chake tarehe 8 Machi 20251, yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha haki, usawa na uwezeshaji wa wanawake, hususan katika taaluma za sayansi na uhandisi.
Akizungumza katika maonesho hayo, Mhandisi Kyando amesema kuwa miaka ya nyuma fani ya uhandisi ilionekana kuwa ya wanaume pekee kutokana na mtazamo wa jamii kuwa masomo ya sayansi ni magumu kwa wanawake. Hata hivyo, kwa sasa kumekuwa na maendeleo makubwa ambapo wanawake wanajihusisha kikamilifu katika sekta hiyo, wakichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi.
“Nimekuwa nikifanya kazi za kiuhandisi kwa miaka saba TANROADS makao makuu, kisha nikawa Msimamizi wa Kitengo cha Mipango mkoani Iringa na sasa ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro,” amesema Mhandisi Kyando. “Kwa kweli, majukumu haya yanawezekana kwa Wanawake kama wakijipanga vizuri katika kazi na maisha ya nyumbani.”
Mhandisi Kyando amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha haki, usawa na uwezeshaji wa wanawake vinazingatiwa. Ameeleza kuwa serikali imewekeza katika utoaji wa fursa kwa wasichana kusoma masomo ya sayansi, huku wakandarasi wanawake wakipewa nafasi kupitia miradi ya barabara.
“TANROADS inahakikisha kwamba asilimia 30 ya bajeti ya mkoa inatolewa kwa wakandarasi Wanawake. Hii ni sehemu ya sera ya serikali inayolenga kuwainua wanawake katika sekta ya ujenzi,” amesema.
Katika Mkoa wa Kilimanjaro, asilimia 37 ya wafanyakazi wa TANROADS ni wanawake, wengi wao wakiwa wahandisi wanaosimamia miradi mikubwa na midogo ya matengenezo ya barabara. Hili ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma, na linaashiria maendeleo katika ushirikishwaji wa wanawake kwenye sekta ya ujenzi.
Mhandisi Kyando amewahimiza wasichana na wanawake kutozubaa bali kuhakikisha wanajiongezea ujuzi ili waajiri wao waweze kuwaamini zaidi na kuwapa nafasi za uongozi. Anatoa wito kwa wanawake kuhakikisha kuwa wanatumia fursa zilizopo ili kuchangia maendeleo yao binafsi na ya taifa kwa ujumla.
“Kwa wale ambao ni viongozi, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunaimarisha haki na usawa kazini, na kuwahamasisha wanawake kushiriki kikamilifu katika sekta ya ujenzi,” ameongeza.
Akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour, na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta, Mhandisi Kyando amesisitiza kuwa ushirikiano wao umechangia kufanikisha juhudi za kuwainua wanawake katika sekta ya uhandisi.
Akiwaalika wananchi kutembelea Banda la TANROADS katika maonesho hayo, amesema wahandisi wanawake watakuwa tayari kutoa elimu kuhusu ujenzi, ukarabati, usalama wa barabara, na masuala mengine muhimu.
“Tunawakaribisha wananchi wa Arusha na mikoa jirani kama Kilimanjaro, Tanga, na Manyara kutembelea banda letu la TANROADS ili kupata taarifa muhimu zinazohusu sekta ya barabara,” amehitimisha.
Kauli mbiu ya mwaka huu "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji".

Mhandisi Motta Kyando