Kasian Lumato
New Member
- Jun 20, 2024
- 1
- 0
Miaka ya nyuma kidogo ilikua ni changamoto kubwa kuona wanawake wakishiriki kwenye siasa , lakini siku za karibuni sio jambo jipya sana japo Bado ushiriki wao sio wa kuridhisha lakini tumeona kwenye nafasi mbalimbali za kijamii, mashirika na taasisi na hata siasa wanawake wakifanya vizuri.
Kwenye Siasa tumeshuhudia wanawake mbalimbali wakishika nafasi mbalimbali kwenye nchi yetu na hata kimataifa mfano: Getruda Mongela, Anna Makinda, Dr Asha-Rose Migiro, Profesa Annah Tibaijuka na hata Sasa Rais Samia Suluhu Hassan hao ni baadhi kwenye siasa lakini pia tumeona wanawake kama Ruth Zaipuna (NMB) Wakionyesha mafanikio makubwa walipopewa nafasi kwenye eneo la uongozi.
Kuhusu changamoto za kijinsia hasa kwenye siasa nadhani changamoto zipo lakini zimepungua kwani baadhi ya mikoa na majimbo yaliyokua yakidaiwa kuongoza Kwa unyanyasaji wa kijinsia tumeona yakichagua wanawake kwenye nafasi za uwakilishi mfano:
Bunda Mjini (Esther Bulaya) , kaliua (Magdalena Sakaya ) na Tarime mjini(Esther Matiko) hii inapaswa kuwa chachu kubwa Kwa wanawake wengine wenye ndoto za kisiasa hasa kujiamini Kwa kujiunga na vyama vya siasa na kuchukua fomu wakati ukifika, kujiandaa vizuri kisera na kimkakati ukweli ni kwamba ukiwa na sera nzuri hakuna Atakae angalia jinsia yako na mwisho kabisa kujikubali wao wenyewe na kuamini katika uwezo walio nao.
Naamini kabisa haya yakifanyika basi tutegemee wanawake wengi wakiingia kwenye nafasi za uwakilishi katika chaguzi zijazo . Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa

Upvote
4