Ni ukweli usiofichika kwamba idadi ya wanawake duniani ni kubwa kuliko ile ya wanaume,kutokana na jarida la Islamic Research Foundation(IRF) la India lililochapishwa mwaka 2009 lilieleza kwamba nchi ya India pekee ndo ilikua na idadi kubwa ya wanaume ukilinganisha na ya wanawake,nchi nyingi za ulaya na Marekani zilikua na idadi kubwa ya wanawake ikilinganishwa ya wanaume. Mimi naamin kabisa kwamba ni kwa sabab hii ya wingi wa wanawake ambapo Mungu akatoa ruhusa wanaume kuoa zaid ya mke 1,na vitab vitakatif vinaruhus wake zaid ya 1 ila kuna baadh ya viongoz wa dini wamekataza wafuas wao wasiwe na wake zaid ya 1. Swali kwa wazaz ni; una mtoto wa kike ambae amefikia umri wa kuolewa,je utamruhusu aolewe matara ili aepukane na uhuni au asiolewe kabisa ili akuletee wajukuu wasio na baba? Na kwa bahati mzuri nchi zinazofuata tamaduni za kuwa na wake zaid ya 1 ndo zinazoongoza kwa kutokua na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa Ukimwi. Watu wanaoamini kile kinachoitwa HAKI ZA BINADAM wanadai kuwa na mke zaid za 1 ni kumnyima haki mwanamke,mda mwingine tunatakiwa kufanya kama madaktar ambao wanaukata mguu wa mtu mwenye kansa ili kumsaidia kuokoa uhai,kwa mfano huo kuoa wake wengi ni kuwaokoa na sio kuwatesa. Ila ifahamike pia kwamba sio kila aitwae mwanaume anaweza kuwa na wake wengi,ni wale tu wenye sifa za kuwahudumia ipasavyo. Vijana tujitokeze kuoa wake zaid ya 1 ili kuwasaidia dada zetu na sio kuishia kuwaita kwa majina yasiyopendeza kutokana na kukosa ndoa.