CHIEF MALUGU
Member
- Jun 7, 2024
- 10
- 12
WANAWAKE WAWEZESHWE KUWA NA NGUVU YA KIUCHUMI, ILI KUONGEZA USHIRIKI WAO KWENYE SHUGHULI ZA SIASA
Kwa Mujibu wa wikpedia inatafisri Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali za jamii, kama vile mji, taifa, au hata dunia nzima (siasa ya kimataifa).
Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.
Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.
Ushiriki wa wanawake katika siasa nchini Tanzania umekuwa na changamoto kadhaa, lakini kuna maendeleo yanayoonekana kadiri miaka inavyosonga mbele.
Katika uchaguzi wa 2015, inaelezwa wagombea wanawake walishinda 204 kati ya kata 3,946 (5.2%) mwaka 2015.” Wabunge wanawake 25 walishinda uchaguzi wao kati ya viti 264 (9.5%), wabunge 5 wanawake waliteuliwa na Rais kati ya viti 10 na wabunge 2 wanawake walichaguliwa na Baraza la Wawakilishi. Katika Bunge la Kitaifa viti 145 kati ya 393 vimeshikiliwa na wanawake ambayo ni (37%) tangu 2015.
Takwimu mbalimbali kutoka vyanzo tofauti tofauiti vinaonyesha kwamba ni 30% tu ya wanawake wanaoshikiri kwenye shughuli za kisiasa nchini Tanzania.
KWANINI WANAWAKE WENGI HAWASHIKIRI KWENYE SHUGHULI Z A SIASA NCHINI TANZANIA
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kuelezea kwa nini wanawake wengi wanaweza kuwa ugumu wa kujihusisha na masuala ya siasa, pamoja na mtazamo wa kijamii kuhusu ushiriki wao katika nyanja hiyo:
Mfumo wa Kijamii na Utamaduni:
Katika baadhi ya jamii, jukumu la wanawake limejikita zaidi katika majukumu ya nyumbani na familia.Hususani jamii za kifugaji na wakulima na maeneo mengine ambayo bado hayawaamini wanawake.
Mila na desturi zinaweza kuwa na athari kubwa sana katika kuwazuia wanawake kujihusisha na siasa au kushika nafasi za uongozi.
Ubaguzi na Ubaguzi wa Kijinsia, Mazingira ya Siasa
Mazingira ya siasa yanaweza kuonekana kuwa yana ushindani mkubwa, ugumu wa kifedha, na mifumo iliyojengeka ambayo inaweza kuwakatisha tamaa wanawake wasio na uzoefu au rasilimali.
Ubaguzi katika Uteuzi wa Vyama vya Siasa;
Vyama vya siasa vinaweza kuwa na mifumo inayopendelea wagombea wa kiume au wasio na historia ya wanawake katika uongozi, hivyo kuwafanya wanawake kupata ugumu katika kupata nafasi za uongozi.
Mifumo ya Elimu na Upatikanaji wa Rasilimali;
Wanawake wanaweza kukabiliwa na changamoto katika upatikanaji wa elimu ya kutosha au rasilimali za kifedha ambazo zinahitajika kwa kampeni za uchaguzi au ujenzi wa kazi ya kisiasa.
Kuna sababu nyingi na hizo ni chache kati yao.
NINI KIFANYIKE?
KUWEZESHA KIFEDHA/KIUCHUMI
Kutoa ufadhili na rasilimali za kutosha kwa wanawake wanaotaka kugombea. Mara nyingi wanawake wanakabiliwa na changamoto za kupata fedha za kampeni ikilinganishwa na wanaume, hivyo kuwezesha ufikiaji wao wa rasilimali hii ni muhimu sana kwa sababu wanawake wengi wanakabaliwa na tatizo kubwa la kiuchumi hivyo serikali na wadau wengine wanaweza kuangalia namna ya kupunguza au kuondoa vikwazo vya Kiuchumi kwa
Hii inaweza kujumuisha kuboresha sheria za uchaguzi, kutoa fursa sawa za ufadhili wa kampeni, na kuboresha mazingira ya kisheria yanayowahusu wanawake, Hapa nitatoa mfano wa vikwazo vya kitaasisi Kupunguza Gharama za Kuwania Uongozi, Sheria zinaweza kubadilishwa ili kupunguza au kutoa msamaha ada za kusajili wagombea(fomu za kuwania nafasi hizo). Hii itapunguza mzigo wa kifedha kwa wanawake wanaotaka kugombea na hivyo kuwapa nafasi sawa na wanaume.
Kuwa na mfuko maalum wa kuwawezesha wanawake wanaotaka kujihusisha na siasa hasa siasa za majukwaani nah ii iwe kwa vyma vyote vya siasa. Ruzuku wanayopata Msajili au sheria itamke wazi kwamba ni lazima vyama hivyo view na pgogram maalum au mfuko maalum wa kuwawezesha wanawake kushiriki shughuli za siasa.
Pamoja na hayo wabunge wa viti maalum wanawake wawe ni wenye umri mdogo mfano kuanzia Miaka 21-25 tu lengo ni kuwapa uzoefu kisha waachie nafasi hizo kwa wanawake wengine, Historia inaonyesha wkamba mwanamke akishateuliwa kwenye viti maalum kwa muhula mmoja anakuwa tayari ameshazoea na kama sula la kiuchumi anakuwa na uwezo, hivyo kwanza jambo hili litafanya wasichana au wanawake wadogo kuhamasika kuingia kwenye siasa.
MAMBO MENGINE YANAYOWEZA KUFANYIKA KUONGEZA IDADAI YA WANAWAKE KWENYE SHUGHULI ZA SISA NI PAMOJA NA,
Kuongeza Kiwango cha Uwakilishi wa Wanawake: Kuweka vigezo vya uwakilishi wa wanawake katika nyadhifa za uongozi kama vile kugawanya viti kwa uwiano wa kijinsia au kutoa miongozo ya kisheria ambayo inahimiza vyama vya kisiasa kuteua wanawake kwa nafasi za uongozi.
Kuboresha Taratibu za Uchaguzi: Kuhakikisha taratibu za uchaguzi zinazingatia usawa wa kijinsia na kutoa miongozo juu ya jinsi ya kuhakikisha usawa huu unazingatiwa kikamilifu wakati wa mchakato wa uchaguzi.
Kupinga Ubaguzi na Unyanyapaa: Kupambana na ubaguzi na unyanyapaa dhidi ya wanawake wanaojitokeza kwenye siasa. Kuelimisha umma na kuchukua hatua kali dhidi ya aina zote za unyanyapaa ni muhimu kwa kujenga mazingira ya kujiamini kwa wanawake.
Pamoja na sababu zote hizo bado naamini kwamba Wanawake wakiwezeshwa kiuchumi, itaongeza kiwango au idadi ya wanawake wanaoingia kwenye siasa na Kufikia malengo ya Malengo ya Dunia yanayohusu uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi Ambayo yanalenga kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.
Hii inamaanisha kutaka usawa kamili wa kijinsia katika maeneo ya maamuzi ya kisiasa na uongozi, ili wanawake waweze kushiriki kikamilifu na kwa uwiano sawa na wanaume katika mifumo ya kisiasa na uongozi kote ulimwenguni. Lengo hili linajumuisha vyama vya kisiasa, serikali za kitaifa na za mitaa, taasisi za kimataifa, na mashirika ya kijamii kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi sawa za kushiriki katika maamuzi yote ya umma.
IMEANDIKWA NA KALEBO MUSSA MALUGU
kalebomussa82@gmail.com

Upvote
10