informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Makamu Mwenyekiti wa Umoja Wa Wanawake Tanzania (UWT) Zainab Khamis Shomari ametoa wito kwa Wanawake na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya madini ikiwemo kuwekeza kwenye shughuli za uchimbaji pamoja na kutoa huduma migodini.
Amedai kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa kila mtu kushiriki katika uchumi wa madini.
Makamu Zainab ametoa wito huo leo Oktoba 11, 2024 alipotembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bomba mbili Mkoani Geita.
"Sekta ya Madini ina fursa nyingi na Wanawake hawapaswi kubaki nyuma,wakati ni sasa Serikali yetu sikivu imetoa na itaendelea kutoa Leseni kwa kwa wachimbaji wadogo ikiwemo Wanawake, sasa ni muda wa kuchimba kuimarisha uchumi wetu na Taifa kwa ujumla"amesema Makamu Zainab