Wanawake wengi wamejigeuza bidhaa tuishi nao kwa akili

Wanawake wengi wamejigeuza bidhaa tuishi nao kwa akili

Loading failed

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2023
Posts
2,603
Reaction score
7,501
Habari za wakati huu.

Ndugu kuna bidha haramu zisizo lipa kodi na hata nyingine kupigwa marufuku na mamlaka za nchi husika kama tunavyojua na ikitokea ume kamatwa na bidhaa haramu basi adhabu yake inajulikana ndugu zangu.

Kama kichwa cha habari kinavyo sadifu hapo juu naendelea kwa masikitiko huku nikiwaasa wanaume wenzangu tuendele kushi kwa akili na wanawake zetu

Wakuu wanawake wengi sasa wamejigeuza kuwa bidhaa haramu katika jamii zetu huku mlengwa mkuu wa kununua bidhaa hiyo direct au indirect akiwa ni mwanaume kwa kuoa au kwa kutokuoa lazima utanunua tuu.

Ndugu ndoa nyingi sana zinavunjika, zina suasua , zina mitafaruku ya kila namna migumu migumu, na huku vijana wengi wakizidi kukataa kuoa kabisa yote haya yanatokana na wanawake kujigeuza kuwa bidhaa haramu katika jamii zetu.

Ndugu hatari hii ya wanawake kujigeuza bidhaa tumeishuhudia kwa kuona yafutayo:;-

1:Mikasa ya usaliti katika mapenzi

2: Mauaji ya kikatili kwa wapenzi na wakati mwingine mauaji mabaya ya halaiki, matumizi mabaya ya njia za uzazi wa mpango ikiwemo vidonge vya P-2, pamoja na utoaji mimba uliokithiri

3: Wapendwa kuachiana ulemavu wa kimwili, kisaikolojia na kiroho wakudumu

4:Ongezeko la manabii, mitume na walimu wa uongo wanaofundisha maswala ya ndoa na mahusiano kwenye nyumba za ibada, mashuleni, vyuoni , mikutano ya adhara, semina na miadhara mbalimbali huku wakilenga kukusanya maokoto na kujitajirisha binafsi zao

5: Ndoa kuvunjika, watoto wa mitaani, watoto kufanyishwa kazi katika umri mdogo, manyanyaso ya kingono kwa watoto na watu wazima halikadhalika na vijana kukataa kuoa nakuolewa

6: Ongezeko la umalaya , vitendo vya kikahaba, uasherati na vinavyo fanana na hivi vya kumchukiza Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote viijazavyo nchi kwa namna zake na hata kwenye jamii husika kwa imani zao

7: Mmomonyoko wa maadili kuongezeka katika jamii pamoja na ongezeko la watoto wasio wafahamu baba zao na wenye malezi duni

8: Wizi wa makusudi unaofanywa indirect na hawa wanawake zetu, pamoja na ongezeko kubwa la single mother ndani ya nchi husika

9: Kuvunjika kwa umoja katika jamii, nje na ndani ya nchi husika

10: Ongezeko la wanaharakati wa baya katika jamii zetu wenye chuki na husuda kwa wengine kutokana na kuumizwa kimapenzi na wapendwa wao


##Ndugu zangu kupitia athari hizo hapo juu tunaona moja kwa moja jambo hili la wanawake kujigeuza bidhaa limepelekea wanawake wengi kujiweka katika makundi ya bidhaa tofauti tofauti yakiwemo kama ifuatavyo ;-

i) Wanawake waliojiweka bidhaa za makundi ya juu ,

ii) Wanawake waliojiweka bidhaa za makundi ya kati

iii) Wanawake waliojiweka bidhaa za makundi ya chini


***Katika kundi la kwanza ,Ndugu zangu wanawake wa makundi ya juu huku tutapata wale wanaojiuza direct na indirect kwa garama kubwa sana , huku tutapata wanawake pia wanaowakataa wanaume wasio na hela nyingi na mali za kutosha,

Pia tutapata wanawake wenye kuwaka tamaa ya kuolewa na matajiri, kundi hili pia lina wanawake wanaotoka katika familia za kitajiri na walio poteza muelekeo baada ya wazazi wao kupoteza maisha kwa namna moja ama nyingine

Huku tutapata wanawake wake za watu na wasio wake za watu wanao danga na matajiri wakubwa wakubwa huku wakipendelea vitu vya gharama sana mpaka mionekano yao ya gharama sana ndugu zangu wanawake wa kundi hili wengi wao hawana future kabisa za maisha yao kwani hawazingatii sana maswala ya kesho yao pamoja na ndoa zao

Katika kundi hili pia utakutana na wanawake wanaogawa uroda kwenye yale makasino na mahoteli makubwa makubwa nje na ndani ya nchi sehemu tofauti tofauti

Hapa wengi wao wanakua wasafi sana pia wanapatikana kwenye mitandao ile ya dating za hadhi kubwa kubwa, pia kwenye matamasha makubwa makubwa sana huko ndipo utakapo wapata pia wengi wao ni wafanyakazi walioajiriwa kabisa ila wanatamaa mbaya ya hela


***Katika Kundi la pili. Hapa tutakutana na wake za watu wenye maisha ya kati,mama wanyumbani, wanawake wenye biashara zenye vipato vyakati ,tutakutana na mabinti wanaozunguka huku na huko waliojiweka katika kupata na kukosa na huku wakisema labda haikua bahati yao,

hapa utakutana na wanawake wenye vipato vya kati na wasio na vipato vya kati , hapa utakutana na wanafunzi wa vyuo na wasio na vyuo

Pia katika kundi hili utakutana na wanawake wanaotokea vijijini kwenye familia zenye uwezo, utakuta vitoto vya shule vinavyo danganyana kuolewa na matajiri, utakutana na wanawake wengi wanaoishi maisha ya kitamthilia na maslay queen wasio jua hata uchungu wa hela.

Ndugu zangu pia katika kundi hili utakutana na wanawake wanaojiuza kama bidhaa kwenye mitandao ya kijamii , kwenye bar zenye hadhi, hotel ndogo ndogo na kwenye matamasha ya viwango vya kati,

Hapa pia utakutana na wanawake wake za watu na wasio wake za watu waliojificha kwenye nyumba za ibada ila matendo yao huwezi kutarajia ndugu zangu

***Katika kundi la tatu , ndugu zangu hili sasa ndiyo hatari kubwa sana duniani na katika jamii

Hapa utakutana na wanawake wanao omba ila hawajui waliombalo, masikini wanawake na mabinti zetu Mungu awa rehemu

Kundi hili ndiyo limepelekea vijana wengi kuchagua kukataa ndoa na kujiunga chaputa, kundi hili linazingatia maokoto sana siyo kawaida na katika kundi hili kumejaa vibinti vidogo sana vingi vinazagaa sana mitaani nyakati za jioni na usiku,

Katika kundi hiki pia utapata dada poa wengi wanaojipanga barabarani na kwenye mabar uchwara ndugu zangu

Ndugu zangu kwenye kundi hili utakutana na wanawake wasio eleweka , wasio jua thamani ya mwanaume , wadangaji, waongo sana, wezi, na wenye tamaa ya vitu vizuri vizuri pasi na kujua pahala pakuvipatia , wanawake wa vigodoro na wanawake wasio sikivu kwa wazazi wao na mafundisho ya kweli hawataki kuyasikia

Kwenye kundi hili kwa masikitiko utakutana na mabinti wa kwanzia darasa la 4 nakuendelea mpaka sekondari, utakutana na wanawake wasio nakazi ila hujui wana ishije, utakutana na single mother wengi wakujitakia, utakutana na vibinti vikiwa vimebebana ma watoto bila kujua baba zao halisi ni wakina nani ,

Pia wanawake wavivu wa kazi, kufikiria na kujituma wanapatikana hapa wote

Wanawake wa kundi hili hawana future kabisa ya maisha, wengi wao utakutana nao wakiwa wamevaa mayeboyebo yale makubwa makubwa, viatu vya manyoya vikubwa kupita saizi zao, nusu uchi huku wamefunga dailek kichwani, wengi wao wanatoka kimapenzi na wavuta bangi wakizani ni ujanja wa maisha kumbe wanaangamiza roho na miili yao

Ndugu zangu wanawake wa kundi hili asilimia kubwa sana wanatoka katika familia masikini au zenye malezi ya mama tuu, na kama ni malezi ya wazazi wote basi utakuta baba yake ni mlevi sana au mvuta bangi.

Ndugu zangu wanawake wakundi hili hawaangalii hela kubwa kubwa hapa ukiwapa chochote kitu kama malipo ya bidhaa yake basi unatunukiwa pasi na yeye kujali chochote

Wala swala la maradhi ( magonjwa ya zinaa ) wao kwao haliwapi tishio lolote.


$$$ Ndugu zangu, wazazi wetu, Taasisi za kidini na zisizo za dini, jamii kwa ujumla na taasisi za kimaadili mpo wapi . Je hamuyaoni haya au ndiyo mtatuambia ni utandawazi pamoja na ugumu wa maisha?

$$$ Wanaume tupo wapi na tunafanya nini, sauti zetu kali na nzito za kukemea zipo wapi, wanaume tunafanya nini kama vichwa vya kuongoza hawa waliotokana na ubavu wetu?

$$$ Wanawake wenye maadili je, mpo wapi na mnafanya nini kusaidia hili na kuwa kemea vikali wanawake wenzenu wanaowadhalilisha?

Nb: UZI HUU HAUFUNGAMANI NA KUKASHIFU WANAWAKE WALA IMANI YA MTU BALI UPO KWA LENGO LA KUSEMA UHALISIA ILI JAMII BASI ICHUKUE HATUA ZA HARAKA
 
Kwani umelazimishwa kujihusisha na msichana/mwanamke katika jamii ulimoo. Ka humudu game kaa kandoo
 
Kwani umelazimishwa kujihusisha na msichana/mwanamke katika jamii ulimoo. Ka humudu game kaa kandoo
Kwa masikitiko na sikitika kukuambia ukweli kwamba wewe haupo sawa kisaikolojia na una hitaji usaidizi wa haraka ili usizidi kuharibu kizazi kilichopo na kijacho
 
Tajiri hasusiwi. Tukiisusia Israel, tumeisusia ulaya na US. Hapo ni kama kulinyonga taifa. Sisi tujikite kuwaomba hamas wawaachie ndugu zetu wawili kisha tuendelee kujenga taifa. Hata hivyo hatuna ushawishi kwa sasa wa kubadili chpchote kilichoamriwa na wakubwa duniani
 
Sijasoma mada ila nimesikitika sana hapo uliposema mwisho wa dunia umekaribia
nilikua sina nguvu ya kusoma ila, nilipoona unasema mleta mada anadai Mwisho wa dunia umekaribia.
Nimepata hamu ya kusoma, because i believe Unyakuo umekaribia. 😁
 
Aiseeeh
Nasubiri michango ya "bidhaa" ninunue🤣
 
Tusipuuze mambo ya msingi, Mwanamke kwa sasa anatakiwa kuwa Makini sana.

Wanaume wameanza mchezo mchafu wa kuharibu nyota za wanawake kwa kufanya nao ngono.
wapo wa naume ambao wapo tayari kutoa mamilioni kulala na Mwanamke bikra, na kuiba nyota yake.

Hedhi ya mwanamke na mimba changa ni diri kubwa kwa sasa.

Ukidanganyika na elfu 20 za kila siku za matumizi bila kujua mwanaume anaiba nini kwako, siku ukijua utalia machozi mazito.

Mathayo 24:11-13
[11]Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
[12]Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
[13]Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
 
Kwa masikitiko na sikitika kukuambia ukweli kwamba wewe haupo sawa kisaikolojia na una hitaji usaidizi wa haraka ili usizidi kuharibu kizazi kilichopo na kijacho
Kisa cha kutuaminisha na kutufanya tuwaone wanake ni bidhaaaanake nn? Changamoto ya kisaikolojia ni pale unapoanza kuwaona wengine hawana thamani ka ulonayo wwe.
 
Kisa cha kutuaminisha na kutufanya tuwaone wanake ni bidhaaaanake nn? Changamoto ya kisaikolojia ni pale unapoanza kuwaona wengine hawana thamani ka ulonayo wwe.
Acha mihemko kaa kwa kutulia kama huusiki, leta hoja nzito upewe nafasi ya kusikilizwa habari ya ushindani acha na kubali maneno niliyokuambia . Sasa kama mwanamke kataa kwa hoja na siyo vinginevyo
 
Nimepotosha wapi
Rudia kusoma mada upya alafu angalia na comment yako ya kwanza alafu kwa mifano hai isiyo pungua 100 uelezee umma kuna uhusiano gani wa mwisho wa dunia na nilicho kiandika?
 
Wanawake, wanawake......wanawake!
Viumbe dhaifu, lakini strong willed.
Si wapambanaji, lakini wana mioyo ya huruma.
Hawapigani lakini ulimi wake waweza kukupiga knock out
Wana maneno mengi, lakini wanaweza kutunza siri yake maisha yote.
Si wachajarikaji sana , lakini wanaweza kuwa na akiba za ajabu!
Na mwanamke akidhamiria kupata kitu kwako, atakipata tu!

Yaani hii ni experience yangu na wanawake tofauti, over the years.

Tatizo moja tu kwetu wanaume, ni kuishi nao kwa akili.
Mwanamke anaishi kwa malengo.
Ukimtongoza tu, kitu cha kwanza utaombwa vocha. Mapenzi yakishamiri basi simu janja kama ya kwako itaombwa.
Mapenzi yakiendelea kuwa matamu basi na kodi ya nyumba mwanaume utalipa.
Ukishtuka na kurudisha nyuma majeshi ndio utaona mwanamke alivyo na akili.
Zitakuja meseji lov lov za kukumissi, na habari za kusikia umepata mwanamke mwingine.
Wanaume tulivyo weak na kulegea, hapo mwana mama atajiachia uweke na mimba kabisa.
Kama mwanaume hukuwa mjanja kuchunguza hiyo mimba, kuna uwezekano kuwa unailea mimba ya Juma, kijana mtanashati aliyeko jirani.

Baada ya mimba, hapo tena mwanamke isha kuwa nyumba ndogo, matunzo yanadaiwa kama nyumba kubwa.

Mtoto akizaliwa copy right na sura yako, wallahi tafuta kiwanja.
Uanze kumjengea bibie hata chumba kimoja.
Na kwa wanaume tulivyoumbwa, majukumu ndiyo yanapamba moto.
Mama si tu ni tegemezi bali sasa una ndoa mbili.
Jamani maisha matamu, lakini machungu.
Wasalaam Aleikhum, Wabarakatu!
 
Back
Top Bottom