Hii ishanitokea kwa wadada watatu tofauti, mdada anakutafta yeye mwenyewe, anakuja yeye mwenyewe, sio kwamba umemfata, na bando lake la simu anatumia kukupigia, tena mtu hauko sehem ya biashara, uko zako gheto, anakuomba muongee dili halafu anakupa ofa ya tsh laki 3, laki 5 au laki 2 kwenye dili analo-propose, anakwambia siku flani anakuletea hela, siku ikifika, subiri MTU subiri na wewe, hakuna jibu..tena bora akwambie amebadilisha mawazo, siku ikifika jitu linakaa kimya..kwahiyo dili inakufa hapo hapo, dili ulokuwa unaitegemea haifanyiki, na hela hupati
Wadada mnapenda vitu feki feki, kama huna hela si useme? Kuliko umsubirishe MTU hewani, kama ww mdada unajijua huna hela, unatoa ofa ya nini??? kuna mdada hapa natamani nimpigie simu nimtukanee matusi yote..simdai ila kaweka ahadi ya kutoa hela siku flani hlf hajatimiza , wala kauli ya kuvunja hio ofa hajanipa.. Huu sio ustaarabu..
Tafuta hela kutegemea pesa isiyokuwepo mfukoni mwako utakufa na pressure, afu usitegemee mwanamke ktk maisha yako.
afu wadau wengi hamjamuelewa mtoa mada ana maanisha nini, ishu ni kwamba yeye ni mfanyabiashara sasa katika kufanya biashara wadada wengi ambao wanakuja kama wateja wanatamani huduma au wanunue bidhaa na wakati huo hawana pesa, sasa wanaweka ahadi wafanyiwe moja mbili watalipa, sasa unakuta anawaandalia fresh kwa kutumia gharama ya muda saa ingine hata pesa yake mfukoni afu mwisho wa siku hawaji wanashindwa sasa.
Hii kitu hata mi kwenye biashara ishanitokea wakuu msimlalamikie mdau tu, maana mi binafsi nilikutana na demu mmoja yeye ni superstar hawa maslay queen tena alikuwa kwenye mashindano ya umiss akaniambia nimuandalie kazi fulani ana ofa atatoa kama laki 3 hivi nikafanya kazi kweli kumbe hana kitu anasubiri danga atume pesa na danga hatumi, kkmbuka nishagharamika muda wangu na pesa yangu ya mfukoni siku nzima nimempambania aisee iliniuma sana.