Wanawake wenye watoto wadogo msifadhaike.

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Wote ni wazima niende moja kwa moja kwenye mada.

Hutokea pale mama anapokuwa na mwanae katika shughuli fulani sherehe, ofisini, safarini n.k.
Mtoto hutokea kumchangamkia mtu ambae hata mama hakutegemea kama inaweza kuwa hivyo na wakati mwingine hadi mama wa mtoto kujishtukia na kufadhaika kuwa mwanae ameleta usumbufu mahali hapo ila nakwambia HAPANA mwanao hakuleta usumbufu wowote.

Hii imekuwa ikinitokea japo na kichwa kichafu na sura mbuzi ila nimekuwa na urafiki mkubwa sana na watoto wadogo kwenye nyanja tofauti na wakati mwingine hata marafiki zangu wamekuwa wakishangaa hili.

Ni kweli kuna watoto uchagua mtu wa kumchangamikia ila kwangu namshukuru Mungu watoto wengi uchukua hata dk 2 kama yupo karibu na mimi najikuta tayari ni marafiki wakubwa na huwa napenda kuw hivyo.

Huwa imetokea mara nyingi tu wakati mwingine hata naweza kujua kabisa mama wa mtoto anajishtukia nakuona kama usumbufu kwa "uncle" kama na wewe upo karibu na watoto basi jina halitakuwa geni kwako.

Nimeleta uzi huu baada ya kuona ni wengi tu wanawake hufadhaika na kuona ni usumbufu labda "uncle" atakuona mwanao hukumpa malezi bora anapokutana na watu ila nawapa facts kuwa huwa tunafurahi sana na hatuhisi kitu chochote kibaya.

Tunajua pale ndio wakati wa wewe kupumzika maana tabu vurugu mnazokutana nazo na muda wote unakuwa nae wewe narudia msifadhaike.

Wengine hata wanapoona mwanae kamchafua "uncle" au kamkojolea wanauzunika ila hamtaki kufanya hivyo hamna usumbufu wowote ule ndio maana tunapenda kucheza nao.

Japo wanawake wengi wameweka nadharia ya kuwa wanaume kutokana na hizi sura mbuzi sura nyani ni kunyamazisha watoto kwa kuwatisha.

Ila kama ndugu yangu nawe unapenda kuwa karibu na watoto ila usiogope kuitwa "uncle" popote pale unapomuona mtoto usisite kumpa tabasam na mbwembwe zingine utajiongeza.
Ila mtoto mdogo kila mtaa kila mahali atakuwa rafiki yako.
Hapa sura mbuzi kichwa kichafu ila moyo wa pipi tuwatunuku watoto.

Naimani hata ambao mmeoa mnaweza kutumia hivi vitu kuwa karibu na wanao.


Nawasilisha wakuu
 
Sawa kabisa. Hata mimi napenda sana kubeba watoto wadogo, ni furaha na amani. Hata hivyo kuna akina mama wengine hawapendi kabisa wanao wabebwe ba watu wasiojulikana au na watu hovyo. wengine wanajitetea watoto wataambukizwa maradhi mbalimbali kama vile ugonjwa wa ngozi.

Ila kuna wabeba watoto wengine wanakera, akishika mtoto tu kitu cha kwanza busu, na wengine wanaenda mbali hadi kumpiga denda mtoto. Wakati huo unakuta mtu mwenyewe hata mswaki hajapiga, mwingine amekula ugoro wake au pombe inakuwa ni kero tu.
 
Ila kuna wabeba watoto wengine wanakera, akishika mtoto tu kitu cha kwanza busu, na wengine wanaenda mbali hadi kumpiga denda mtoto. Wakati huo unakuta mtu mwenyewe hata mswaki hajapiga, mwingine amekula ugoro wake au pombe inakuwa ni kero tu.

Hahahaha hawa ndio hawajielewi kabisa na wanasababisha kubaniwa wenye nia njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…