Wanawake wenzangu wenye vitanzi (IUD), mnaendeleaje?

 
Mkuu mchezo mtamu ila matokea ya ule mchezo sio matamu naogopa sana mimba alooh 😭
Situation kama hizi nawaonea sana wivu wanawake wa kizungu wenzetu wanaeleweka kiurahisi na wenza wao, shughuli iko huku sht holes countries
Kwa sisi waafrika mwanamke bado anachukuliwa kama " chombo cha starehe" na kazi yake ni kutimiza matamanio ya mwanaume bila kujali hisia au afya ya mwanamke huyo. Ni hivi punda afe mzigo ufike. Wanaume wanakuzwa na fikra hizo na wanawake wanakuzwa na fikra kwamba wao ni vyombo vya starehe na wanapaswa kutimiza haja za wanaume wao hata kama wao wataathirika. Ndio maana inatakiwa watu wazungumzie masuala haya kabla hata ya kufunga ndoa,matarajio yajulikane. Mimi binafsi pamoja na baba mjengo tuliongea hili suala kwa undani kabla ya kuoana,mimi nilikuwa nafahamu kwahiyo nilianzisha mada . Halafu tukajifunza wote kwa pamoja ( tulipata mwalimu online) alikuwa mwanamke na tuliomba nafasi ya kusikia kutoka kwa mume wa huyo mwalimu jinsi gani yeye kama mwanaume analichukulia hilo swala na anakabiliana na changamoto zinazojitokeza. Pia wao binafsi walipata fursa ya kuongea kivyao( man to man). Ilisaidia kwa kweli. So tulifunga ndoa tushajua what to expect.
 
Sawa
 
Naskia kuna njia za asili jaribu tumia izo
 
Tunaoomba tuelezee vizur hiz methods za asili ulizotutajia
 
UTI ni maambukizi kwenye mfumo wa mkoji na IUD inawekwa kwenye mfumo wa uzazi
Sasa vinaingilianaje
Kitanzi hakisababishi UTI moja kwa moja bila kinaongeza hatari kwa sababu bacteria wanaweza kuweka makazi pale ya kudumu kisha bakteria hao wakawa wanahama mara kwa mara na kusogea kwenye njia ya mkojo na kuleta maambukizi. Katika hili kitanzi kinakuwa kama makazi ya bacteria kitaalamu wanaita " biofilm".
 
Ivi ni kweli kutoshiriki muda mrefu kunapelekea maumiv ya mgongo na kiuno hasa ukiwa period
 
Tunaoomba tuelezee vizur hiz methods za asili ulizotutajia
Mimi nayotumia inaitwa Billings Ovulation Method au BOM kwa kifupi,kwa njia hii unachunguza ule ute unaotoka kwenye via vya uzazi kwa kuhisi tu " unajiskiaje" mfano unyevu, ukavu,utelezii, etc. Pia unaweza kuuchunguza kwa macho au hata kuushika kama bado hujawa mzoefu wa kuchunguza unajiskiaje. Ukishajichunguza na kujua kama uko kwenye siku za kushika mimba au siku salama then unaepuka tendo la ndoa kama hautaki kushika ujauzito kwa wakati huo. Njia nyingine zinahusisha teknolojia kama vile kupima homoni kwenye mkojo kwa vipimo unavyoweza kuwa navyo nyumbani au kupima joto la mwili kwa themometa maalum inawekwa mdomoni. Teknolojia hizi hurahisisha mwanamke kujua kama yuko kwenye siku za kushika ujauzito au lah kisha yeye mwenyewe atafanya maamuzi kulingana na anataka kushika ujauzito au kuzuia ujauzito.
 
Ivi ni kweli kutoshiriki muda mrefu kunapelekea maumiv ya mgongo na kiuno hasa ukiwa period
Self control sio rahisi kipenzi ila inahitajika maana kuna kipindi mume ataumwa,atasafiri kutafutia familia n.k. Kama huna self control huku mume ameenda kuhangaikia familia labda kasafiri mwezi au miezi miwli utafanyaje?
 
Wana pesa za kutosha kulea,wewe unazo?
Hujanielewa hoja yangu.
Nimemkatalia jamaa kwamba kuwa na watoto wengi kunapoteza muda wa kufanya biashara. Hivyo akimaanisha wafanyabiashara waliofanikiwa hawataki au hawawezi kuwa na watoto wengi.
Personally nilihitaji watoto wawili tu.
 
Mkuu mchezo mtamu ila matokea ya ule mchezo sio matamu naogopa sana mimba alooh 😭
Situation kama hizi nawaonea sana wivu wanawake wa kizungu wenzetu wanaeleweka kiurahisi na wenza wao, shughuli iko huku sht holes countries
Watu sikuhizi mnaogopa mimba kuliko ukimwi😅

Hapo dawa ni kuolewa na mwanaume mkae mbalimbali! Tofauti na hapo atakubaka kwa lazima😆
 
Sawasawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…