Wanawake. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Kwasababu leo ni siku ya wanawake duniani naanza kwa kuwapongeza wanawake wooote wa hapa jamvini na uraiani ntawapa salamu zao kadiri ntakavyoweza.
Happy woman's day to all of you ladies. Being a woman might sometimes seem like a really hard task but we are gifted with all the strength, power, knowledge, beauty, caurage, patiance, love and kindness to make it . . .all we have to do is USE those things WELL.

I love being a woman, a woman is all I need to be.

Nwy......
Hamna msemo nisioupenda kama ule wa "WANAWAKE HAWAPENDANI" even though una ukweli mwingi ndani yake. Just last week nilikuwa najibishana na rafiki yangu kuhusu huo msemo, nikakataa katu katu kwamba sio wanawake wengi , na pia hata wanaume wapo wasiopendana vile vile. Siku ya pili nikiwa na rafiki yule yule tulikua tumesimama mahali tunasubiria kitu wakapita wadada wawili na wote nikawagonga na mfuko niliokua nau-swing back and forth. Wa kwanza akaniomba mimi samahani na mimi ni nikamwomba vile vile, yule wa pili nikamwomba mimi na rafiki yangu pamoja tukiwa tumepishana sekunde kadhaa, hakutikia yangu akaitikia ya rafiki yangu (mkaka). Bila kupanga nikajikuta nimesema tu "hmmmm mbona kapokea samahani yako na yangu kaiacha?!" .Rafiki yangu akasema "ahhhh we sinimeshakwambia hampendani!!!!?" Mwenyewe nikabaki kusema "I guess you were right" huku nikijisikia mnyonge kwa kuishia kukubali kitu ambacho binafsi hakinifurahishi.

Kinachonishangaza ni kwamba baadhi ya wanawake katika jamii yetu wanapenda sana kubwebwa (wale waosapoti msemo wa "TUKIWEZESHWA. . . . . " even though wako kwenye position za kujiwezesha wenyewe) , ila wanapomwona mwanamke mwingine amejiwezesha iwe ni kifedha, kielimu, kitaaluma au hata kisanaa wanaMCHUKIA badala ya kufurahi kwaajili yake, au hata kumuonea wivu na kujishughulisha kufika kule alipo yeye.
Ukiachilia mambo makubwa hayo kuna vile vitu vidogovidogo(Petty stuff) vinavyowasumbua baadhi yetu. Utakuta mtu hata hamfahamu mwenzie ila anasema "Yule fulani namchukia kweli." Ukimuuliza kwanini utasikia " Ahhhh anajisikia sana. Ona anavyovaa/ona hata tembea yake." n.k Yani mtu akivaa kiatu/nguo/panga nyumba/nunua gari ya ghali zaidi basi tabu. Akiwa na mume/mwenzi anaemheshimu, mjali na kumpenda/akiwa na familia inayoendelea vizuri kwa kila namna badala ya kumu-ADMIRE na kujifunza hili au lile toka kwake anamchukia. . .

Kwanini tunaona/fanyana maadui kwasababu ya jinsia? Yatupasa tujifunze kuchukua yale mazuri tunayoyaona/tamani kwa wenzetu na kuyatumia kama changamoto. Tuyatumie kufika walipo wao au hata mbali zaidi kama wafanyavyo wengi wa kaka zetu.

Usimchukie mwenzako kwa kuwa na kile unachotamani, acha majungu, umbea na mengine yote yasiyo na faida kisha ujishughulishe. Kama ni bahati kila mmoja amejaaliwa yake, ila hamna ambae inamfuata akiwa amelala, bali kila mmoja anatakiwa kukimbiza yake mwenyewe.

"Bahati ya mwenzio usinunie. . .tafuta yako".

Happy woman's day ladies. Be blessed!
 
Aksante sana QoMMU
Kwanza hongera na pili neno lako kuntu!
 
Namshukuru sana mama yangu kwa kunizaa kidume aka beberu la mbegu
Kila nikifikiria angeniweka kwenye rambo na kunitupa jalalani leo hii sijui ningekuwa sisimizi!
Pongezi za dhati zimwendee mama angu mzazi popote alipo bila yeye hivi vitamu nisinge kuwa nakula kabisa.
Na wanawake wengine kuweni na roho ya huruma kama mama angu.
Mtoto wa mwenzio nae ni mwanao msinyanyase watoto wa kambo wanyanyaseni baba zao kwa kupiga mimba sehemu sehemu mtoto hana kosa jamani ila huyo mdingi ndo mwenye kosa.
Big up maza
 
Kweli bana, yaani wanawake wakichukia basi wana chuki mbaya sana hata kwa mtoto ambae hana hatia. (hapa naongelea baadhi ya wanawake)

ofu topik: kumbe leo sikukuu ya wanawake? ndo maana huyu waifu wa jirani kavaa nguo mpya kumbe
 

Mama yako ni jasiri Fidel. . .treat her like one.
 
Kweli bana, yaani wanawake wakichukia basi wana chuki mbaya sana hata kwa mtoto ambae hana hatia. (hapa naongelea baadhi ya wanawake)

ofu topik: kumbe leo sikukuu ya wanawake? ndo maana huyu waifu wa jirani kavaa nguo mpya kumbe

Lawyer inabidi tuanzishe ka-movement cha kuhamasisha hiyo chuki hata ipungue.

Hahaha. . .Wewe mbona hukuniletea zawadi kwaajili ya sikukuu?
 
Lawyer inabidi tuanzishe ka-movement cha kuhamasisha hiyo chuki hata ipungue.

Hahaha. . .Wewe mbona hukuniletea zawadi kwaajili ya sikukuu?
Hii chuki bwana mimi mwenyewe inanishangaza sana kwasababu nilidhani kwa elimu inaweza ikapungua lakini kuna mdada nilimshuhudia ni msomi wa shahada za juu lakini kila nikimpeleleza kiulawyer ulawyer namgundua ana elements za hiyo kitu, sasa sijui hata inatatuka vipi hii kitu?

Zawadi yako naimalizia kuipulizia pafyum, kaa mkao wa starehe.
 
Nadhani ni kiasi tu cha kueleweshana kwamba haisaidii. Kama mwenzake anacho, anacho tu. Hata achukie mpaka apate vidonda vya tumbo bado mwenzie "atakua nacho."

Marashi gani??
Usikute sabuni ya Ayuu. . .
 
Umesomeka!!
 
Lizzy mambo mengine ni nature huwezi kupingana nayo
 
Msema kweli usione tabu kumpongeza, hongera mama kwa kuliona hili 99% umeongea mipoint tupu! ila nadhani tatizo hilo ni ktk matendo ya kike hivyo ni ngumu kupatia ufumbuzi wake!
 
Lizzy mambo mengine ni nature huwezi kupingana nayo
Ina maana kuwa na roho mbaya wewe unaita nature?...
Wanawake wakija kujitambuwa uwezo wao basi wanaweza kuja kuongoza nchi hii
% kubwa ya viongozi wote wa kuchaguliwa wamewekwa madarakni na wanawake, lakini akigombea mwanamke mwenzao hawamchagui.
Majizi yote kwenye ofisi za umma ni wanaume, wanawake ni waadirifu sana sehemu za kazi, inapotokea janamke jizi basi ujuwe hapo kuna mwanaume ndiye aliyemshawishi na siyo plan zake binafsi.
 
ulichosema ni kweli kabisa bi dada.
wanawake wengi wanarudi nyuma kimaendeleo sababu ya kuangali au kuonea wivu
maisha ya fulani . wakati angepoteza huo muda kufikiri kuhusu yeye na yake angefika mbali .

HAta na hivyo nilichogundua kuhusu sisi wanawake.
ikitokea shida yeyeto, hata kama tunachukiana kiasi gani wote tuko
mstari wa mbele kusaidi na tutaongea vizuri tu . ni mimi tu nimeona hilo au ?
 
well.... as some say!! WE ARE BACK TO MEN'S DAYS.... :rant::rant::rant:
 
Lizzy!
Mie nakubaliana na hao wanasosema wanawake hatupendani
Ni wachache sana wenye roho ya tofauti.
Ukiona mwenzio ana hiki unanuna - badala ya kujiuliza kapata vipi na mie nifanye juhudi
Mwenzio akikuzidi unanuna badala ya kuwaza na mie nifanyeje..
Lakini bado tunapenda na tunasaidiana inapobidi
 
Hao wanawake wa hivyo mnakutana nao wapi? Mie mpaka muda huu bado sijamkuta wa hivyo

Btw: Sioni uhusiano wa wanawake kutopendana na mwanamke mmoja kutoitikia samahani moja kati ya mbili alizopewa kwa kosa hilo hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…