Wanayanga tufikirie kubadili rangi ya jezi yetu sasa

mwanapolo

Senior Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
193
Reaction score
56
Wana Yanga wenzangu, nafikiri umefika wakati sasa wa kubadili rangi ya uzi wetu ili uendane na wakati bila kubagua utashi wa mtu.

Nimeamua kutoa dukuduku langu hilo kwani inamuwia vigumu sana mpenzi wa chama cha upinzani kuvaa jezi ya Yanga mtaani. Kama ilivyo rangi ya jezi zetu ndio rangi inayotumiwa pia na chama cha Magamba.

Kwa mapendekezo yangu ni kuwa tutumie jezi ya rangi ya njano tukiwa nyumbani na jezi ya mchanganyiko wa njano na nyeusi tukiwa ugenini. Bendera zetu, rangi ya jengo, rangi ya kadi na vitu vingine vibaki kama vilivyo kwani tusipoteze kabisa asili ya rangi yetu.

Nakumbuka hata tumempoteza mwanachama wetu ambaye ni Mbunge wa ubungo kwa ajili ya rangi ya jezi na ushangilaji wetu.

Mungu ibariki Yanga Afrika, Mungu ibariki Taifa Star
 
Kuna Jezi nakumbuka ilitumika mwaka 1993 kama sikosei wakati wa fainali ya kombe la CECAFA kule kampala na Yanga ilitwaa ubingwa,
Nadhani ile ndiyo inafaa sasa kutumika.
Siku hizi ukivaa jezi za Yanga huishi kuzomewa mtaani, eti Magambaaaaa.
 
Wana Yanga wenzangu, nafikiri umefika wakati sasa wa kubadili rangi ya uzi wetu ili uendane na wakati bila kubagua utashi wa mtu.

Nimeamua kutoa dukuduku langu hilo kwani inamuwia vigumu sana mpenzi wa chama cha upinzani kuvaa jezi ya Yanga mtaani. Kama ilivyo rangi ya jezi zetu ndio rangi inayotumiwa pia na chama cha Magamba.

Kwa mapendekezo yangu ni kuwa tutumie jezi ya rangi ya njano tukiwa nyumbani na jezi ya mchanganyiko wa njano na nyeusi tukiwa ugenini. Bendera zetu, rangi ya jengo, rangi ya kadi na vitu vingine vibaki kama vilivyo kwani tusipoteze kabisa asili ya rangi yetu.

Nakumbuka hata tumempoteza mwanachama wetu ambaye ni Mbunge wa ubungo kwa ajili ya rangi ya jezi na ushangilaji wetu.

Mungu ibariki Yanga Afrika, Mungu ibariki Taifa Star

Tumieni hii ndio nzuri
 
Rangi za Yanga ni bomba hazihitaji mabadiliko, Magamba ndiyo watafute rangi zao, hata hivyo kwa nini tuhusishe michezo na siasa? Huyo mbunge wa Ubungo naye kama kapotea eti kwa sababu za rangi hajui alilolitenda, mbona Sarungi, Sumaye na Kapuya ni wana Simba mahiri na wanamagamba wanaotinga Njano na Kijani majukwaani?
 
pia inakuwa vigumu kutofautisha kati ya yanga na ccm pindi ukutanapo na m2 amevaa kijani na njano.
 
Hii inakera sana hata ukizingatia ushangiliaji ule wa ccm..ccm....kwa kwel unapoteza kabisa kwan kuna wanayanga weng ambao si wanamagamba.hvyo viongozi wetu wajaribu kulifikiria hlo kwan yanga ni club na haimilikiwi na chama chochote cha siasa.
 
Rangi si hoja, maana ndivyo ilivyoanzishwa.Ila hiyo shangilia ya magamba siizimii kabisa.
 
Hiyo alianzisha hoja ni mwana CCM.Kwani kwenye mpira tunavaa jezi au makombati!!!!!!!!!!!?Wanaoshangilia CCM!!CCM!! ni wanayanga au Simba!!?Ukivaa mikombati yako kwa kujidai mshabiki wa yanga ukipigwa Simo!!!!!!!!!!!!!!!!!

Back
Top Bottom