Wanda Nara: Mwanamke mpambanaji mwenye jicho la kina Raiola na Mendez

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Kamwene wadau wangu wangu wa JF.

Kuna riwaya moja ipo pale Form Five na Six inaitwa Vuta N'kuvute ebhana ni moja ya love story iliyojaa ufundi mkubwa sana wa sanaa ya uandishi. Kwa wale walosoma HKL, HKL wataelewa ninachosema; nyie mliosoma PCM kuna chand [emoji6]. Hiyo riwaya ukiangalia dhamira ya mapenzi na mahusiano imeguswa kinagaubaga sana, nenda katafute usome halafu umkumbuke mwanadada Wanda Nara.

Ukizunguka pale Ufaransa utakutana na mitaa yenye mataa na mnara mkubwa na mrefu sana pale katikati ya jiji, napo si pengine ni Paris. Kuna chama la wana linaitwa PSG.

Pale PSG Kuna kiumbe mmoja wa kuitwa Mauro Icardi [emoji1544][emoji1544].Yes, huyu ni streika matata sana ambaye amekichafua sehemu nyingi sana.

Ukienda kule Argentina yeye na Paulo Dyabala mitaani kwao wanaheshimika hata zaidi ya Messi na wanaamini wao ndo Messi wao na madogo wengi wanajiita kina Icardi au Dyabala.

Nani asiyeujua uwezo wa Icardi katika kufumania nyavu? Lakini hakuwa na maisha mazuri sana akiwa Inter Milan na hata timu yake ya taifa na mara nyingi skendo yake na Wanda Nara ilitawala sana kuliko hata kipaji chake.

Wanda ni mke wa Icardi kwa sasa lakini alikuwa ni mke wa Maxi Lopez ambaye kipindi wapo Sampdoria ilitokea mwanamama akamuelewa mzee wetu fundi wa mpira Icardi.

Ilitokea msuguano sana na kitu hicho kilimfanya Messi amchukie na akatoa amri kwa kocha asiwe anamjumuisha kwenye timu ya taifa, na hi ilitengeneza bifu kati ya Messi na Icardi.

[emoji1544]Lakini unaambiwa mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika. Mtoto Wanda akamuelewa jamaa, wakadumu mpaka Icardi alivyotoka Sampdoria mpaka safari yake ya PSG mwanadada hakuonesha ajizi ya upendo wake kwa fundi wetu huyu.

Wanda amekuwa mwanamke mwenye upendo sana kwa mume wake na mpaka jamaa akamfanya awe wakala wake .

Wakala na kichuna wa Icardi, Wanda amempambania sana mume wake kutoka pale Inter kwani baada ya jamaa kuporwa kitambaa cha unahodha. Ilisemekana wasingemuuza na wala asingepata nafasi ya kucheza kwani alikuwa hana nidhamu Wala hakujituma akiwa na kikosi cha Inter.

Lakini Wanda kupitia ushosti wake na mke wa mkurugenzi mkuu na rais wa PSG akawaita hotelini, akawaambia shemeji yenu kule analetewa za kuleta embu ongeeni na majamaa tumlete goalgetter huyu chap aje aungane na akina Mbappe na kina Di Maria bila kuwasahau kina Neymar.

Dili lilikaribia kukwama lakini unaambiwa wakati bwana ake anapasha gym, mke wake na wakala wake alikuwa hana hata muda wa kuegesha kichwa, kujibebisha alihakikisha mteja wake anapata timu.

Wakati jamaa akiwa hana hili wala lile, simu iliingia ikimtaka akafanyiwe vipimo tayari kwa kukichafua PSG na ilikuwa ni mida ya lala salama.

[emoji1544] Icardi yupo PSG ndiyo lakini kuna mkono mkubwa sana wa mke wetu Wanda Nara pale. Mwanamke anaepambana kama kina Mino Raiola na akina Pogba wao au akina Mendes na kina Ronaldo waoo[emoji1544][emoji1544][emoji1544].

Licha ya kuwa mapenzi yanatokea na kuanza popote bila kujali utachukuliwa vipi na jamii kikubwa na mapenzi ya dhati, lakini jiulize mke wako anawaza kupambana upate pahala pa kujibanza au naye anasubiri tu upambane ulete nyumbani[emoji1550][emoji1550][emoji1550][emoji1550].

 
Utajiuliza kwa nini Messi na Maradona wanamchukia Icardi? Mardona aliwahi kumwambia kocha wa timu ya taifa ya Argentina wewe ukimuita Icardi timu ya taifa na wewe ni msaliti tu kama yeye.

Huyu jamaa haya mambo ya skendo na ugomvi ulianza hivi alipofika italia kucheza mpira wa kulipwa kwa mara ya kwanza alifikia club ya Sampdoria huko Italia katika mji wa Genova, wakati huo huo kuna muargentina mwenzake akampokea kama ndugu wametoka nchi moja anaitwa Maxi Lopez.

Maxi kipindi hicho anakaa na mke wake huyo Wanda Nara. Maxi na mke wake waligombana wakaachana na wakati huo nafikiri walikuwa na watoto wawili. Mauro akachangamkia fursa akamchukua shemeji yake na hapo hapo ndiyo akapata pia uhamisho wa kutoka Sampdoria kwenda Inter Milan ( Club ya mji wa Milan).

Ugomvi ukawa mkubwa kwa sababu Icardi akawa kama anamrusha roho rafiki yake kwenye mitandao anamponda halafu anarusha picha akiwa na watoto wa Maxi, kitu ambacho Maxi alikuwa hataki ni kile cha watoto wake kutangazwa hovyo mitandaoni.

Kipindi hicho sasa Maxi na Ex wake wana kesi yao mahakamani kama wanandoa mke alimshitaki mume kwa masuala yao ya ndani. Kama kawaida ya mapenzi tena Wanda nara ndiyo akawa amefika kwa Icardi na wakapata watoto wengine familia ikaongezeka, na kwenye mitandao kama kawaida mke kumponda ex wake kuwa hajali watoto wake, na Maxi alikuwa anajibu kuwa hakuwa anapewa muda wa kuwaona watoto wake kila mara Wanda anakula bata na tu na Icardi.

Ugomvi ulikuwa mkubwa mpaka club zao zikikutana Maxi alikuwa hapokei mkono wa Icardi na mashabiki wa Sampdoria walikuwa wanamtukana pia Icardi kama msaliti.ikawa kama kugongelea msumari wa moto sasa icardi akamuweka Wanda Nara kama wakala wake kwenye masuala ya mikataba ya michezo.Kwa ujumla matukio ni mengi mno ya hawa watu watatu mpaka kisa cha icardi kuanza kusugua benchi na kupokonywa kitambaa cha unahodha.

 
Malaya tu huyo.
 
Eeh bwana ex wife wa dani alves alifanikisha dili gani za uwakala ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ex-wife wa Dani Alves bi Dinara Santana ni moja wa popular sporting agents kutoka Brazil na pia vile vile ni bonge la mjasiriamali huko kwao.

Huyu amekuwa ni wakala wa Dani Alves tangu 2006 na ndio aliyewezesha dili la Dani Alves kutoka Sevilla kwenda Barcelona na baadae Juve,PSG na sasa Sao Paolo.

Pamoja na wawili hao kutalakiana mwaka 2011 lakini wameendelea kuwa bega bega kwenye sula zima la kibiashara na malezi ya watoto wao.

Bi Santana amekuwa ndio akishughulika na endorsement deals zote alizonazo Dani Alves katika career yake mpaka hapa alipofikia.

Mbali na Dani Alves pia vile vile Bi Santana amekuwa akifanya kazi na wachezaji wengine wa kibrazil kama Fabinho,Willian na Gabriel Paulista.

Wateja wake huwa wanamsifu sana kwa ukachakarikaji wake pale anaposimamia deal, maana huwa anahakikisha wameridhika kabisa.. kwanza huwa anakutafutia yeye nyumba utakayoishi kulingana na hobby ulizonazo mbali na mpira, kama wewe unapenda golf basi lazima nyumba atakayokutafutia iwe na uwanja golf.

Pia vile vile anafanya kazi na kampuni ya michezo ya kijerumani ijulikanayo kama KICK & RUN kwa upande wa amerika ya kusini.

Kiufupi tu huyu mwanamama ni jembe sana tumpe hongera zake single mother huyu mchakalikaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah hapa dani alves hajamuacha kijumla itakuwa?hivi wanaume watoto wangapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliachana mazima Dinora akapata mwanaume mwingine wakaachana tena, sasa hivi hana mume, kinachowaunganisha sasa hivi yeye na Dani Alves ni kazi tu na kushirikiana kwenye malezi ya watoto wao wawili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Namkubali sana dani toka yupo sevila sijawahi kusikia relationship yake ndio Leo nashukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…