Wandugu nisaidieni kupambanua hili

mwathu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2012
Posts
403
Reaction score
210
kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikijiuliza na kushindwa kupata jibu au kung'amua wapi ambapo elimu ya Tanzania imekwama. Kimsingi mimi nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ya themanini na wakati nasoma elimu ya msingi hasa nikiwa Tanga sikuliona hili lakini tangu nilianza sekondari Dar es salaam,A level Tabora na hatimae undergraduate degree pamoja na masters nimegundua kuwa kuna tatizo kubwa miongoni mwetu katika kusoma na kuandika.

Watu wamekuwa kwa mara nyingi sana wakitamka kimakosa au kuandika kimakosa maneno mbalimbali hasa yenye mchanganyiko wa herufi R na L. utakuta mtu neno Haraka anasema halaka, karibu anasema Kalibu, pia utakuta neno lima mtu anasema rima, kula anaandika kura yaani mpaka inakuwa kero.

Hili tatizo nilikuwa nikiliona kwa watoto ila kwa sasa mpaka waandishi wa habari, watangazaji wa redio na luninga wanatangaza kwa makosa ambayo yanachosha hata kuendelea na habari hizo. Mtangazaji yuko very smart anashindwa kusema na kutofautisha matamshi ya neno hafla, ghafla.

Naomba wadau mnisaidie kama na nyinyi mmefanikiwa kuliona hilo tatizo na ni kweli tuna tatizo kwa waalimu au maana nashindwa kuelewa wandugu lakini tunajenga kizazi kibaya kisichojua hata kutamka vizuri maneno.
 
ELIMU BIASHARA KUSOMA KUFIKIA MALENGO KUKESHA MBWEMBWE km Mulugo hajui maana YA TANZANIA NA NI NAIBU WAZIRI WA ELIMU unazan product yake n ip? angalia juu kuna watu sahihi alaf njoo chin huku utapata majb yake mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…