Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
Huyu bwana mdogo hajaingia uwanjani tangu january 2022 kwa sababu alikua na kesi ya kumtia vitasa demu wake hii ikapelekea Manchester United kumsimamisha kazi. Hatujamuona uwanjani tangu kipindi hicho na haijulikani anarudi lini. Kwa sasa anafanya mazoezi ya pekee yake nyumbani akifuatiliwa kwa ukaribu na wataalamu wa afya na mazoezi wa Manchester United pamoja na kupewa miongozo ya kimbinu na kocha mkuu Erik ten haag huku akisubiri hatma yake. Anarudishwa kwenye timu, anauzwa au anatolewa kwa mkopo?
Dogo kashamalizana na msala wake ila bado Manchester United hawajamrudisha uwanjani, nafikiri wanasubiri hili suala lisahaulike kidogo kambini na kwenye media, kumrudisha dogo haraka wanahofia itasababisha mgawanyiko katika timu. Taarifa za ndani zinasema timu ya wanaume wakiongozwa na captain Bruno hawana shida dogo kurudi uwanjani kikwazo ni timu ya wanawake. Kwa alichomfanyia mwanamke mwenzao hawa wakina dada hawataki hata kumuona kwenye viunga vya Carrington.
Nitafurahi sana nikimuona tena dogo uwanjani. Greenwood ana spidi nzuri, anajua kuwatoka mabeki pinzani, anapiga mashuti mazito kwa miguu yote, ana shabaa ya kulenga goli. Pamoja na faida ana mapungufu yake pia, mwili mdogo kiasi cha kushindwa kushindana nguvu na mabeki wa kati endapo akicheza streika wa kati, sio mzuri wa mpira wa vichwa, mchoyo wa kutoa pasi akifika eneo la mpinzani yaani analazimisha kupiga hata akiwa kwenye eneo baya wakati angeweza kumpa mpira mwenzake ambae yupo eneo zuri.
Mpaka Greenwood anasimamishwa mara nyingi alikua anapangwa kama mshambuliaji wa pembeni akitokea upande wa kulia eneo ambalo kwa sasa anacheza Antony. Kutokana na Antony kuzingua mara kwa mara kila anapocheza watu wengi wamekua wakitamani Greenwood arudi uwanjani kuchukua nafasi yake wakifikiri ndie atakuwa mkombozi wa timu au upgrade kubwa ya Antony kitu ambacho wanajidanganya.
Kabla dogo hajasimamishwa kazi mpira wa Manchester United ulikua ule ule tia maji tia maji. Alikua na baadhi ya moments nzuri lakini hakuwa shujaa wa kuibeba timu yeye binafsi kama ilivyokua kwa Rashford baada ya fainali za world cup mwaka jana. Bado ni kijana mdogo ana nafasi ya kuboresha kiwango chake lakini ukweli ni kwamba Greenwood sio world class, sio generational talent ni mchezaji mzuri wa kawaida. Akirudi atasaidia kwa kiasi chake lakini ujio wake hautakua hit kama ujio wa Salah pale Liverpool au ujio wa Haaland kwa jirani, Manchester City. Tumuombee dogo arudi uwanjani lakini tupunguze matarajio makubwa kwake.