Imani (Faith)
To believe with all our heart in our people, our parents, our teachers, our leaders and the righteousness and victory of our struggle
Leo ndiyo tunamalizia sherehe zetu za kwanza. Tunawasha mshumaa wetu wa mwisho kwenye KINARA chetu na kuandaa KARAMU kwa wale tuwapendao. Baada ya karamu, tunakaa na kutafakari maana ya neno IMANI katika jamii yetu ya watu weusi. Tunajiuliza tulikotea wapi hadi hapa tulipofika. Tunawazungumzia waliotutangulia, wakina; Kinjikitile "Bokero" Ngwale, Mkwavinjika Munyigumba Mwamuyinga ( Chief Mkwawa), Shaka, Frantz Fanon, Aime Cesaire,Dedan Kimathi Waciuri,Waruhiu Itote (General China), Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, Leopold Senghor, W.E.B. DuBois, Malcolm X, Martin Luther King, Soledad Brothers, Marcus Garvey,Thomas Sankara, Steve Biko, Malkia Nzinga Mbande, Sojourner Truth, Harriet Tubman bila kuwasahau walio bado nasi wakina; Angela Davis, Desmond Tutu, Nelson Mandela n.k. Ni wakati huu ndiyo inabidi tuwaulize babu zetu, bibi zetu, wazazi wetu kuhusu huko walikotoka. Ni wakati huu inabidi tuangalie wenzetu na kujipa moyo kuwa saa ya mapambano ni sasa! Kuwa pamoja na wakina Gabriel Mugabe, tutafika huko tunakoenda na siku moja tutaweza kuamka na kusema bila kusita kuwa " mimi ni mtu mweusi, mwana wa Afrika na utanikubali kama nilivyo maana ndivyo nilivyo na sivyo unavyotaka niwe".
Baada ya kutafakari hayo, tutazima KINARA chetu na kungoja siku ya kesho na kesho kutwa zitatuletea nini, sisi wana wa Afrika. Tutazisubiri bila kuwa na wasi wasi maana tunajua kuwa hatuko peke yetu kwenye mapambano haya maana tumetoka mbali, na waliotutangulia wako nasi, na iko siku tutafika mwisho wa safari yetu!
Amandla...........Wana wa Afrika! Amandla.......