Wangekuwa shuleni,wasingekuwa barabarani

Wangekuwa shuleni,wasingekuwa barabarani

albuluushiy

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
1,404
Reaction score
686
Miaka kadhaa iliyopita wakati bado nipo sekondari (shule ya upili), nilikuwa nikipata wakati na wanafunzi wenzangu kuelezana maisha ya nyumbani mbali na yale ya kuonana na kukaa darasani kila siku asubuhi hadi mchana. Mara nyingi wakati huo Mwalimu hayupo darasani ama hamna kipindi, ndio tunapata muda wa kubadilisha mkondo wa mawazo kwa kuibua mazungumzo yoyote mbali na masomo yetu ili kuiweka akili yenye afya zaidi.

Nayakumbuka vyema maneno ya mmoja wa rafiki yangu (wakiume), aliwahi kuniambia kuwa kama si vile kuja shule kila siku basi wakati ule tunapiga soga au Mwalimu yupo darasani anasomesha, basi yeye angekuwa na jembe shambani yuko katikati ya tope au dongo gumu analima. Alikuwa na maana kuwa ugumu wa maisha yake na familia usingemruhusu kukaa nyumbani bila ya kupewa jembe, ingembidi tu atoke na jembe ili awasaidie wazazi katika kilimo chao cha kimsikini.

Kuna vijana Jumamosi ya wiki iliyopita walisababisha taharuki katika maeneo ya Sinza, Tabata, Magomeni na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam. Huenda wengine wapo vituo vya Polisi sasa, ama wengine wapo mitaani wakijipanga kufanya uhalifu mwengine, au wanauguza majeraha waliyoyapata kutoka na kukimbizana na Polisi kwa wakati huu.

Niliposoma habari kuhusu Mohamed Ayubu kijana wa miaka takribani 19 ambaye mwili wake ulikutwa na majeraha ya kupigwa maeneo ya Tandale akiwa tayari ameshaaga dunia, kisha habari ile inasema kuwa Ayubu aliacha shule na kujiingiza katika vikundi vya kihuni, basi moja kwa moja nilimkumbuka rafiki yangu.Kumbe hata Ayubu kama angekuwa shule basi asingekuwa miongoni mwa Panya Road.

Rafiki yangu alinambia kuwa kama si shule basi yeye angekuwa anatoka na jembe kila siku asubuhi kuelekea shamba, aliamini kuwa kwake yeye ile ni adhabu hasa akizingatia kuwa jembe analolitumia si la trekta bali ni la mkono, hivyo shule ilikuwa inamuepusha na kazi ile aliyoiyona ni ngumu. Umasikini si sababu inayokubalika kuwa wewe ndio uwe na haki ya kupora na kuiba kwa nguvu.

Wakati mwengine usilazimishe wizi kuwa ndio ukuingizie kipato cha kila siku, mwisho wako ni kuchomwa moto, watu wengine hata wanaroga. Unaweza kuumwa maradhi hayana tiba kila hospitali uwendayo kumbe laana za Mungu. Kama umekuja Dar es Salaam kutafuta maisha na upo miaka mingi na mambo yanaenda kombo basi rudi kijijini ukaanzishe kilimo Kaka yangu.

Nguvu zako za kubeba mapanga ni bora na kheri sana kama utaenda kubeba jembe. Sisemi haya kwa dharau na kejeli lakini kwa akili yangu nahisi kwenda kijiji ukaanzisha kilimo au mifugo ni bora zaidi kuliko kukaa Dar kuvuta bangi, kupora na kuharibu mali za watu. Utakufa! Rudi kijiji maisha si mjini tu, japo mchicha utakusaidia. Ukimuona Bakhresa na wengine basi usidhani kuwa wamekuwa vile kwa sababu ya kukaba, wameanza chini sana hata ukielezwa walikoanza unaweza usiamini.

Wengi wa Panya Road ni vijana wadogo ambao wakati ule wanatembea na mapanga, nongo, bisibisi,sime,m arungu barabarani basi walitakikana wawe wako katika maandalizi ya kushona nguo zao, kutafuta madaftari mapya ili kurudi shule kwa mwaka mpya wa masomo 2015 au wawe katika muhula (semester)ya kwanza mwaka wa pili au wa tatu chuoni wakisubiri mitihani ya mwisho wa semester.

Inaweza kuwa hali ya kimaisha imemfanya mtu aache shule lakini haijawa sababu ya kuwa na haki ya kuiba. Nirudie kusema kuwa maisha sio Dar es Salaama tu. Unaweza kwenda kuhamia Korogwe, Bariadi, Kanyarwe (Bukoba), Misungwi (Mwanza), Vigwaza na Mzenga (Pwani) na kufanya jambo la maana kuliko kuiba, kupora na kuharibu Manzese na Kinondoni.

Mambo hayo ya kishenzi hayatokupa unafuu wa maisha ila utaishi kuchomwa moto tu. Vijijini ardhi zina mbolea za kutosha, huenda peembejeo za serekali zikakufikia, miradi ya "kilimo kwanza" na ufugani wa wanyama na nyuki huenda yakawa ndio mambo ambayo yatakutoa hapo ulipo, si lazima ung'ang'anie Dar.

Kama umasikini ndio unakupa akili za kuiba basi hayo sio maisha na wala hizo sio akili, usitegemee kuwa serekali hii ya Bongo itafika siku moja ikushike mkono katika kijiwe chako cha Mbagala au Ilala cha kuvuta Bangi na kukwapua ikakupe ajira. Serekali wenyewe masikini inadaiwa, kila mwaka inasamehewa madeni, watu wanatia umasikini nchi.

Usitegemee kuwa serekali ndio itakukomboa kama hujafanya juhudi zako binafsi .Fanya juhuidi binafsi lakini sio juhudi za kunyang'any'a. Hazitokufikisha ! Kwa upande mwengine, kila mtu analo jukumu kuhakikisha matatizo haya yanaondoka, nadhani haya ni matatizo ambayo yanasababishwa na kuchanganyikiwa (kisaikolojia) kutokana maisha magumu aliyonayo ama madawa ayavutayo.

Yawapasa wazazi watambue watoto wao wanalala wapi, wanakula nini, isijekuwa baada ya ugali na matembere ya mchana pia naye anaenda kula unga wake ambao si ugali. Kisa cha Ayubu kinaonesha wazi mapungufu ya wazazi katika kufuatilia nyenendo za kijana yule. Mtoto lazima ujue anacheza wapi na marafiki zake ni akina nani na akiondoka nyubani maeneo yake ni wapi.

Ayubu aliacha shule lakini hazikuonekana juhudi za wazazi kumrudisha. Watoto wengine huacha shule bila ya sababu za msingi, anaamua tu kuacha na kisha mzazi hachukui juhudi za kumrudisha. Kaacha na yeye anamuacha kama alivyo acha, jamani huo si ulezi ni ufugaji. Mtoto anatakiwa alelewe sio kufugwa, malezi ya mtoto yawe ni tofauti na ufugaji wa Ng'ombe kama wale wa Wamasai.

Ngo'mbe anapewa kula na kutafutiwa pa kulala. Mtoto yeye anatakiwa apewe kula na kufuatiliwa nyenendo zake zote, kama nilivyosema anacheza wapi, rafiki zake ni nani. Hapo utapata mtoto ambaye si Panya Road Lakini mtoto kumuacha tu afanye atakalo, aingie ndani muda atakao hata saa saba za usiku, mchana kutwa hujuwi kaenda wapi, yupo na nani, wapi na anafanya nini.

Wewe unampa kula tu na kitanda, hapa ukweli utazalisha Panya Road na Mbwa mwitu. Mtoto anatakikana anyooshwe mpaka anyooke sio kuachwa mwsiho wa siku ndio matokeo yake yanakuwa mabaya. Inasikitisha vijana wadogo hata miaka ishirini wengine hawajafika ndio wameshika mapanga mitaani wakikata kata watu kama tungule.

Kwa upande wa Serekali nanyi munapaswa kuonesha juhudi zenu za ziada kutatua tatizo hili, kukamata tu haitosaidia sana mutazima mwaka mmoja wakizaliwa na kukua mwaka mwengine watoto kama hawa, wanaingia tena mitaani. Nyinyi munajua zaidi sababu za watoto hawa kuwa mitaani na njia zipi munaweza kuwasaidia, lakini kubwa zaidi ni kuchanganyikiwa .

Njaa inachanganya jamani madawa nayo ndio hivyo hivyo. Wasaidieni. Elimu ni jambo la msingi, wazazi wahakikishe watoto hawaachi shule kwa sababu zisizo za msingi. Japo wapo wenye elimu ndio hao wanaoiba mabilioni ya pesa lakini wapewe elimu wakiiba mabilioni tutajua jinsi ya kupambana nao huko juu.
 
sawa lakini suala linabaki pale pale kwa nini hawako shuleni..
 
Ujumbe mzuri ila inabidi tuangalie chanzo na sio matokeo. Kwa maoni yangu chanzo kikuu ni;
1. Sera mbovu za serikali kuhakikisha vijana wanapata elimu na nyezo za kuanzia maisha.
2. Mwamko wa wazazi kwenye swala la elimu, inawezekana mzazi asiwe na elimu sana au hajasoma kabisa lakini anajua umuhimu wa elimu na anafanya jitihada zote kijana wake apate elimu bora. Na kuna wazazi wengine wapo kinyume cha hapo.
3. Kujitambua kwa vijana, miaka 19 ni mingi sana kwa kijana kutojitambua. Kuna vijana wana miaka 15 na wanajielewa na kutambua wanataka nin kwenye maisha. Ila kukaa na kuwaza kufanya uhalifu usiokuwa na mantiki huko ni kutojitambua.
4. Malezi; hata kama familia inaishi maisha ya kimasikini ila malezi bora ni msingi wa ustawi wa familia bora. Kuwalea watoto kwenye maadili yanayofaa na kutomuweka Mungu pembeni.

Nini kifanyike;
1. Elimu ndo msingi bora hasa kwa vijana wadogo, iwe elimu ya ufundi, ujasiriamali au ya kawaida. Serikali ifanye kidato cha sita ndo kiwango cha chini cha elimu Tanzania. Pamoja na hayo elimu ya ufundi itiliwe mkazo kwa wale wasioweza kuendelea na elimu ya juu. Mwisho wa siku wapewe mazingira bora ya kujiajiri.
2. Wazazi turudi nyuma tuangalie wapi tumekosea kwenye malezi ya watoto wetu. Kuwalea kwenye misingu imara ya maadili na dini.
 
Back
Top Bottom