Wangui na Wambui (murder probe)

luangalila

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
6,346
Reaction score
6,928
Wakenya na wana jumuiya wote habarini za mishemishe, nimekuwa nikifuatilia hii kesi kwa siku ya tatu sasa kwa wale msio tambua, kuna kifo cha binti mmoja kule Nairobi Kenya ambae ameuliwa na rafiki yake mara baada ya kugundua ana tembea na bwana wake.. binafsi kesi hii ili nifanya niingie gharama kidogo za kuweka mbs ili kupata story about it ila kuna jambo la kujifunza hapa kutokana na kisanga kilichotokea infact hawa mabinti majina yao yananichanganya ila najua kuna mary na judy judy is the one who murdered au sio wa KE ?
 
Hawa kina dada zetu na mama zetu saa zingine huwa siwaelewagi. Nani angeamini kwamba Judy Wangui angemuua mwenzake Mary Wambui na kutupa mwili wake kwenye dimbwi la maji lisaa limoja baada ya kulishana nyama na kujivinjari pamoja? Sio jambo la kawaida kwa mwanaume kuficha hasira na chuki dhidi ya mtu mwingine virahisi hivi. Wakati wa ngumi ni wa ngumi, yakiisha yanaisha kweli.
 
Kwa sakata yote hii nalaumu njemba lenyewe, ameingilia mchezo wa watu bila kuzingatia vigezo na masharti.
Kuchepuka kunahitaji ujanja na utumiaji wa akili, halafu hakikisha mchepuko wako anaelewa nafasi yake, asije kujichanganya wala hata siku moja, aelewe kwa vyovyote vile yeye ana mpaka wake na haruhusiwi kuvuka hadi kwenye kumi na nane za mkeo.
Huyu jamaa alitundika picha zake kwenye ukuta wa mchepuko wake, wapi umewahi kuskia upumbavu kama huo.
 
Mwana kagonganisha Magari yameuanaa..[emoji23][emoji23][emoji23] Kuchepuka nako kunahitaji akili aiseee... Wife kauliwa na mchepukoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mnajua huyo Judy wangui alikuwa ni muajiriwa wa Mary wambui na mumewe Joseph Kori. Judy alikuwa anauza duka la hardware la Mary Wambui. Judy alimuua Mary,kwa akili zake naona alitaka awe mke kamili. Najiuliza kupangishiwa nyumba ya 60k kenyan shillings hakutosheka ???Au alitaka ahamishiwe kabisa kwenye kasri la Joseph Kori ?
 

Hakujua nafasi yake, mtu katolewa kwenye umaskini halafu akaanza kuzingua.
 
Alimuuaje?na ilijulikana vipi yeye ndio muuwaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakikuyu na mali(pesa) ni damu damu ila kibaya wenyewe kwa wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alimuuaje?na ilijulikana vipi yeye ndio muuwaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Cctv camera zimeconferm na tax driver alieitwa na Judy ili amsadie kutoa mwili kwenye nyumba amesema. Kwanza Judy alienda kwa nyumbani kwa Mary,then wakaenda kula nyama choma baadae wakaenda kwa Judy. Inasemekana Kwa Judy kuna picha za Kori all over the wall. Mary alipoona alitaka maelezo,Judy alimpiga Mary na pressure cooker.Inasemekana mara 9.Halafu huyu Judy alimlazimisha msichana wake wa kazi asafishe damu iliyotapakaa ndani. Judy aliomba msaada wa driver anakokodigi magari ili wakautupe mwili kwenye bwawa. Which they did. Uchunguzi bado unaendelea na kesho kesi inatajwa tena.
 
Mama Sabrina Jinsi ilivyojulikana ni mme wa Mary alipoona informations all over the social media ndo akawasha gari kwenda kwenye lile bwawa,polisi nao wakamkamata hapo hapo na wakamwambia ampigie Judy simu ili wakutane home land hotel,maana ni Hoteli ambayo Judy na Mary walionekana mchana wakiwa wote.
 
Hakujua nafasi yake, mtu katolewa kwenye umaskini halafu akaanza kuzingua.
Alitaka ndoa,alitamani Mary aachwe. Hivi unajua hata Mary before alikuwa ni mpango wa kando?Mary nae alimtoa Grace. Inavyoonekana Mary alikuwa si wakutoka ndo maana Judy akaamua kumkatisha maisha.
 
Daaaah aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni wao kwa wao,Unaambiwa hata huyu mary kabla hajawa promoted kuwa wife nae pia alikuwaga mpango wa kando. Mke wa kwanza ni Grace. Joseph Kori alimuacha Grace for Mary. Malipo ni hapa hapa duniani.
Dah!! Kweli malipo hapa hapa duniani mkuu,navuta picha Grace atakuwa anasherehekea kimya kimya.

Jamaa atakuwa anawatembezea koki sana maana iyo mipango ya kando watakuwa wengi tofauti na Judy.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona u tube inasikitisha kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakujua nafasi yake, mtu katolewa kwenye umaskini halafu akaanza kuzingua.
Jombaa blunder ya kwanza aliyofanya Kori ni kuchepuka na rafiki wa karibu wa mkewe. Ila Sielewi Wangui alikuwa na nia gani alipomkaribisha Wambui nyumbani kwake huku akifahamu vizuri kwamba picha za dume wa nyumba zote mbili zilikuwa zipo ukutani na kwamba Wambui angeziona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…