Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Wanigeria wakabiliwa na marufuku ya kutotoka nje ya saa 24 kufuatia maandamano
Maelezo ya picha,Waandamanaji wanapinga gharama ya juu ya maisha na kile wanachosema ni "utawala mbaya"
Mamilioni ya wakaazi kaskazini mwa Nigeria wanakabiliwa na amri ya kutotoka nje ya saa 24 huku kukiwa na maandamano ya nchi nzima kupinga gharama kubwa ya maisha.
Serikali katika majimbo ya Kano, Jigawa, Yobe na Katsina zimewaamuru wenyeji kutotoka nje ya nyumba zao - na kwa hivyo wasihudhurie maandamano - siku ya Ijumaa.
Mamlaka zinasema amri ya kutotoka nje ni muhimu kwa sababu "vigogo" wameteka nyara maandamano ili kupora na kuharibu mali.
Hali ya usalama imeimarishwa kote nchini huku waandamanaji na wanaharakati na waandamanaji wakipanga "siku tisa za hasira".
Katika siku ya kwanza, maandamano katika mji wa kaskazini wa Kano yalivutia umati mkubwa zaidi.
Polisi walifyatua risasi na mabomu ya machozi - na kunyunyizia waandamanaji maji ya pilipili - kujaribu na kuwatawanya maelfu ya waandamanaji. Watu watatu waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine wengi kujeruhiwa.
Waporaji pia walivamia ghala karibu na nyumba ya gavana wa Kano na polisi wanasema tangu wakati huo watu 269 wamekamatwa na kupatikana kwa maboksi mengi ya mafuta ya karanga yenye ujazo wa lita 25 na vitu vingine vilivyochukuliwa.
Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, waandamanaji 13 kote nchini Nigeria waliuawa na vikosi vya usalama katika siku ya kwanza ya maandamano hayo.
BBC