Bodaboda wanavunja sheria nyingi sana na hawako juu ya sheriaHuyu anayetamani kuwa IGP ameshindwa kuwazuia askari wake kukamata vijana wa bodaboda, yaani kwenye mkoa anaousimamia polisi wanaamka Asubuhi wanaingia barabarani kwa ajili ya kukamata pikipiki tu, yaani siyo trafiki au siyo polisi wengine wote kazi yao ni kusaka pikipiki na kuchukua pesa kwa vijana wanahitaji kupata mkate wa kila siku kwa ajili ya familia zao sasa akipewa u IGP sijui itakuwaje
Leo imefanyika hafla ya kumuaga aliyekuwa RPC mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa na kumkaribisha RPC Mpya wa Pwani Pius Lutumo. Wankyo Nyigesa sasa ni RPC wa mkoa wa Kagera ambae amesema anajiandaa kuwa IGP na anaamini maombi yake Amiri Jeshi mkuu ameyasikia. Amedai alijiandaa kuwa DCI na kamishna Zanzibar nafasi ambazo zimeshachukuliwa
Kuhusu IGP aliyepo sasa amesema anaamini anafanya kazi vizuri ila yeye atafanya kazi nzuri zaidi. Wankyo amemuomba Mungu akamuonyeshe Rais Samia na atakuwa amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.
Binafsi naliona picha la kutisha Jeshi la Polisi, subordinate huwezi kutoka hadharani na kudai cheo cha bosi wako tena katika sehemu inayohitaji nidhamu kwenye chain of command kama polisi kisha unabaki na matarajio mtendelea kufanya kazi vizuri, otherwise awe ameshapangwa na bosi wa bosi wake.
======
RPC Wankyo Nyigesa: Nilikuwa najiandaa kuwa DCI lakini nafasi ya DCI ikachukuliwa, nikajiandaa kuwa Kamishna wa Zanzibar wakachukua, sasa hivi najiandaa kuwa IGP, na ninaamini Rais Samia maombi yangu anayasikia, siku moja tafadhali niteua kuwa IGP, Mimi naamini nitafanya makubwa, huwa ninaomba sana Mama siku moja aniote tu halafu anitamke tu niwe IGP, Mimi nitamuomba nifanye miaka mitatu halafu nimwambie Mama Mimi nakukabidhi naondoka unaonaje hapo?,"
"Binadamu lazima uangalie mbele, natamani kuwa IGP, najua IGP aliyopo (Sirro) hajafanya makosa anafanya mazuri lakini Mimi nitafanya mazuri zaidi, matarajio yangu ni hayo, unajua Binadamu lazima uwe na malengo target ya mbele, uwe na ndoto kubwa, huwezi tu kuwa una malengo ya kwamba nitaendeela tu kuwa RPC Mimi nataka kuwa nafasi za Juu, IGP ili nifanye makubwa kwa faida ya Watanzania wengi kuliko Watanzania wa Mkoa mmoja"
"Mimi naamini siku Rais akiniota vizuri anaweza kunipa U-IGP na matamanio yangu ni kuwa IGP, na naendelea kumuomba tu Rais Samia akiona nafaa na akaomba kwa Mungu akamuonesha Mimi sio kwamba atakuwa amekosea yupo sahihi tu, amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.
Pia soma;
Thread 'IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu Dodoma, ACP Mwampakale awa RPC Kagera' Breaking News: - IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu Dodoma, ACP Mwampakale awa RPC Kagera
View attachment 2166233
Kunywa sodaDuuuhhh......akipelekwa Desk Kule HQ Dom atamlilia Nani? Ngoja tuone! Au jamaa alishaweka kambi Mkoa wa Pwani ? As huwezi kutoka Bandari ya DSM Na usipite Mkoa wa Pwani!!!!!!kipolisi Pwani kitovu cha ulaji!!!!!
Hence proved.Soon Siro atampeleka dodoma HQ kusoma magazeti.
Hata kupelekwa HQ amehurumiwa. Alicho fanya ni gross misconduct, he deserved a summary dismissal.Wankyo ni kind of comedian[emoji23]
'Nikiwa igp nitafanya makubwa zaidi' hii ni dharau kwa aliepo. Unatakiwa umhurumie kwa alio yasema, si kumsifu. Alipotoka sana. Bangi zimempeleka pabaya.Kasema vizuri.
Kuna ubaya gani kuwa na ndoto kubwa?
Akwa mfano mimi nikisema siku moja nataka kuwa mkurugenzi wa taasisi nayofanya kazi kuna ubaya gani?
Watu mnataka kumfitinisha Wankyo na Sirro.
Nampongeza Wankyo kuwa na mawazo makubwa na ndoto kubwa ila nimhakikishie hapo alipofika panamtosha.
Kuna mtu hatari sana huwa anamshauri mzee...kuwa flani muweke bench akale mihogo na kusoma magazeti HQ.Soon Siro atampeleka dodoma HQ kusoma magazeti.
Actually huyu mtu ndiyo anaweza kupata favour ya kuwa recommended na Sirro kuwa the next IGP. Alichojaribu kuonyesha hapa ni viision na si kwamba anahitaji cheo cha IGP wa sasa kwa sababu IGP ni presidential appointment,na yeye hana malaka ya kumtoa IGP aliyepo sasa.Aombe IGP Sirro awe hajamsikia au awe amemsikia halafu amempuuzia kwa sababu anazozijua yeye
Utabiri wako umetimia mkuuSoon Siro atampeleka dodoma HQ kusoma magazeti.
YametimiaOne day select Wankyoo hhaaaaaaaa
Ivi kwenye sherehe kulikuwa na K-vant? au waragiii ? au ze doni?
TayariSoon Siro atampeleka dodoma HQ kusoma magazeti.
Hili jambo nimejiuliza na siamini ACP hajui mipaka yake kipi na kipi dio cha kuongea.Dah! Kuna viungo vya kuvichunga sana kwenye miili yetu kwa sisi wanaume! Athumani kichwa wazi, na ulimi!
Yaani dk 0 tu, umeshaharibu kila kitu, halafu yanabakia tu majuto ni mjukuu.
HaaUkiona swala anaringa mbugani
Unajua kanuni za majeshi yetu mkuu?Actually huyu mtu ndiyo anaweza kupata favour ya kuwa recommended na Sirro kuwa the next IGP. Alichojaribu kuonyesha hapa ni viision na si kwamba anahitaji cheo cha IGP wa sasa kwa sababu IGP ni presidential appointment,na yeye hana malaka ya kumtoa IGP aliyepo sasa.
Hili jamaa limeshajifagilia hadi kwa Rais, na kama lina qualifications zinazohitajika; kuna uwezekano mkubwa sana IGP pamoja na Rais wakam-consider mtu huyu kwa cheo hicho. Hata kama ningekuwa mimi kwenye position za watu hawa wawili amabo ndito wanaohuiska na uteuzi wa IGP atakayefuata, ningewenza kumfikiria kwanza huyu jamaa. Kwanza kitu kingine alichokionyesha hapa ni kwamba yuko wazi; napenda watu ambao wako wazi hawakai wameficha ficha siri nyingi rohoni. Huyu jamaa wakimfikiria kwa nafasi hiyo, mimi nitafurahi
Ataipata fresh. Karibu Dodoma, nyamachoma mnadani kila Jumamosi.Duuuhhh......akipelekwa Desk Kule HQ Dom atamlilia Nani? Ngoja tuone! Au jamaa alishaweka kambi Mkoa wa Pwani ? As huwezi kutoka Bandari ya DSM Na usipite Mkoa wa Pwani!!!!!!kipolisi Pwani kitovu cha ulaji!!!!!
Majibu tayari.Kasema vizuri.
Kuna ubaya gani kuwa na ndoto kubwa?
Akwa mfano mimi nikisema siku moja nataka kuwa mkurugenzi wa taasisi nayofanya kazi kuna ubaya gani?
Watu mnataka kumfitinisha Wankyo na Sirro.
Nampongeza Wankyo kuwa na mawazo makubwa na ndoto kubwa ila nimhakikishie hapo alipofika panamtosha.