Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Lindi, inawashikilia watu wanne, akiwamo mtia nia wa nafasi ya ubunge, Ally Chinumba (CCM), kwa madai ya kuwashawishi wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata wampitishe kwenye kura za maoni.
Naibu Mkuu wa Takukuru mkoani hapa, Charles Mulebya, alitoa taarifa za kukamatwa kwa watuhumiwa hao alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana.
Alisema Chinumba alikamatwa juzi Nahukahuka, Jimbo la Mtama saa 11 jioni alasiri wakati yeye na wajumbe wasiopungua (23) wa Halmashauri ya Kata hiyo, nyumbani kwa Ally Chinumba, ambaye ni baba mzazi wa mtia nia huyo.
Mulebya alisema Chinumba ambaye pia ni mtumishi wa Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) makao makuu jijini Dar es Salaam, alikutwa akiwa amewakusanya wajumbe hao kwa lengo la kuwashawishi wampitishe kwenye kura za maoni, ili kugombea kwenye kinyang’anyiro cha ubunge mwaka huu Jimbo la Mtama.
Alisema kwenye gari la mtia nia huyo lenye namba za usajili T.527 DEY (hakutaja aina ya gari) maofisa wa Takukuru walikuta fedha kiasi cha Sh. 841,000 zilizokuwa zimewekwa maeneo tofauti tofauti, zikiwamo bahasha ndogondogo dazani moja zinazohisiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuwekea fedha kwa ajili ya wajumbe husika.
"Gari la mtia nia tulipolipekua, tumekuta fedha Sh. 841,000 na dazani moja ya bahasha ndogo ndogo, bila shaka zilikuwa za kuwekea fedha za wajumbe," alisema.
Alipoulizwa kama wajumbe waliowakuta wanawashikilia, kiongozi huyo wa Takukuru alijibu kuwa wanawashikilia watu wanne akiwamo mtia nia husika, lakini hakuwa tayari kuanika majina ya watuhumiwa wengine watatu.
Alisema Takukuru inaendelea na uchunguzi ili kubaini uvunjifu wa sheria, kwa mgombea huyo kujihusisha na vitendo vya kushawishi wajumbe kwa utaratibu wa kutoa rushwa.
Aliwaonya watia nia wote kwa nafasi mbalimbali zikiwamo za ubunge na udiwani kujihusisha na vitendo vya rushwa, akiwataka wafuate utaratibu, kanuni na sheria zilizowekwa.