Wanne wakamatwa kwa kutengeneza Pombe Kali 'Feki' Morogoro

Wanne wakamatwa kwa kutengeneza Pombe Kali 'Feki' Morogoro

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata Watu wanne ambao ni Ramadhani Mdoe (30) Mkazi wa Msamvu akiwa na wenzake watatu wakiwa wanatengeneza na kusambaza pombe kali feki katika kiwanda kisichosajiliwa (kiwanda bubu) kilichopo Mtaa wa Tushikamane Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.

Watuhuniwa hao wamekutwa na chupa zilizojazwa pombe feki inayofanana na Smart Gin 2544, chupa tupu 2988, chupa zilizojazwa pombe feki inayofananishwa na konyagi 65, chupa tupu mbalimbali za konyagi zikiwa ndani ya mifuko minne, box moja, madumu ya lita 20 yaliyojazwa spiriti 4, pia tupu moja la spiriti, dumu 6 za lita 20 zenye mchanganyiko wa spiriti na maji, dumu moja la lita 13 lenye mchanganyiko wa spiriti na maji, dumu 4 tupu za lita 20, dumu 6 tupu za lita 13 na dumu 6 za lita 13 zenye maji.

Wamekamata pia mifuko 6 ya salfeti na maboksi mawili makubwa yenye maboksi ya konyagi, jaba 3 kwa ajili ya kuchanganya na kuchuja pombe hiyo, gundi chupa 5, PM kwa ajili ya ladha, stika feki 2037 za TRA, lebo 6226 za Smart Gin pamoja na lebo za konyagi kubwa na ndogo 10,886.

Watuhumiwa hawa wanashikiliwa kwenye Kituo kikubwa cha Polisi kwa ajili ya mahojiano kabla ya kufikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi ambapo RPC wa Morogoro, Alex Mkama amesema Watuhumiwa hawa wamekamatwa ikiwa ni
mwendelezo wa misako na operesheni inayoendelea katika Mkoa wa Morogoro, na hii ni kutokana na ushirikiano unaotolewa na Wananchi kwa Jeshi la Polisi baada ya kuwapa elimu ya kutosha kupitia Polisi Kata.

Pia soma - Matumizi ya Kemikali ya Ethanol yanaweza kuathiri ini na kusababisha Saratani
 
Jamaa wapelekwe tbs kupims ubora kama inalewesga serikali iwasaidie wapewe franchise na kampuni husika. Wawezeshwe kama wale vijana wa bashe.
Sema waalizwe biashara walanza lini wadaiwe Kodi.
 
Jamaa wapelekwe tbs kupims ubora kama inalewesga serikali iwasaidie wapewe franchise na kampuni husika. Wawezeshwe kama wale vijana wa bashe.
Sema waalizwe biashara walanza lini wadaiwe Kodi.
Kwani hizi stika za TRA wamezitoa wapi??
 
... maradhi ya koo, figo, ini, utumbo etc yataongezeka kwa kasi sana kwa ufisadi huu wa wajinga wachache kucheza na afya za watu kwa maslahi binafsi!
 
Back
Top Bottom