A
Anonymous
Guest
Licha ya kutangazwa kwa ufadhili wa masomo ngazi ya Master's Degree kupitia Samia Suluhu Scholarship na wanufaika kuorodheshwa kwenye Website ya bodi ya mikopo inayofahamika kama HESLB.
Lakini takribani wiki kadhaa sasa licha ya masomo kuanza ufadhili huo unaonekana wakusuasua ambao haujatoa ufafanuzi na muongozo wa wanufaika takribani 100.
Bodi wamekuwa ni wakutupiana mpira na kuacha watu wakiwa hawajui mustakabdhi na muendelezo ikawa watu walishaaminishwa wajiandae na masomo lakini hakuna kinachotendeka.
Tunaomba Waziri wa Elimu aliingilie kati hili suala ikiwemo kusaidia waahirika hao.
Pia soma ~ Bodi ya Mikopo yasema imetumia Tsh. Milioni 623.2 kuwafadhili wanafunzi wa Masters
Kuna scholarship (Full Scholarship Under Samia Scholarship Program) ilitangazwa na Serikali kupitia Chuo cha Nelson Mandela (Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - NM-AIST) kilichopo Arusha (18/07/2024) kwa Wanafunzi waliopata udahili kwa kozi za Master's pale chuoni.
Baada ya mchakato wa maombi walichaguliwa watu 100 (majina yao yamechapishwa kwenye tovuti ya bodi ya mikopo) na wakaambiwa wajaze taarifa zao kwenye mfumo wa bodi ya mkopo.
Deadline ya zoezi hilo ilikuwa ni tarehe 20/12/2024.
Mpaka leo hawajatoa mrejesho na Chuo cha Mandela kimeshafunguliwa (13/01/2025) na wameshaanza masomo tayari.
Wale watu 100 walishajiandaa kwenda kuripoti chuoni kwa ajili ya masomo na waliomba ruhusa makazini na tayari wameruhusiwa kwa barua (hivo muajiri anatarajia sasa wamesharipoti masomoni) na wengine waliokuwa na fursa zingine za ufadhili hawakuendelea nazo kwani walikuwa na uhakika na hii Scholarship.
Mpaka sasa hawajatupa majibu ni lini wanakamilisha mchakato ili tukaripoti chuoni ukizingatia masomo yamekwishaanza.
Tukiwauliza Bodi ya Mikopo na Chuo cha Mandela hawatupi majibu inatutia mashaka juu ya mustakabali wetu, kwani ni wao waliitangaza na wakatupa utaratibu wa kufanya ila hawakamilishi mchakato ili tukaendelee na masomo.
Tunahitaji majibu ili tukaripoti chuoni tuendelee na masomo kwani tayari tunapitwa masomo yameshaanza chuoni.

=========================