Mnapenda kukuza mambo ambayo hayana tija. Kuna makabila Kenya, nadhani ni makabila mawili, ya Luo na Turkana, ambayo utamaduni wao haukuwa unatambua mambo kama kukatwa govi. Baada ya kushawishiwa na serikali ya Kenya miaka michache iliyopita. Kwamba kuna manufaa ya kiafya ambayo yanaambatana na kutahiriwa wengi wao walijitokeza na wakatahiriwa bure kwenye vituo vya afya. Hamna la ajabu hapo, mimi binafsi sioni ikiwa tatizo kama mtu atachagua kutahiriwa au kukosa kutahiriwa. Govi la akilini ndio huwa lina madhara makubwa kwa maendeleo ya nchi na ya watu binafsi pia. Hayo mengine yote sio ya maana vile.