Mzalendowadamu
JF-Expert Member
- Jul 10, 2016
- 218
- 318
Habari wanajukwaa.
Katika pitapita zangu za mihangaiko nimekuwa nikifuatilia namna ya kupata Madini tajwa hapo juu. lengo langu ni kununua toka nje ya nchi kwa wachibaji wadogo kisha kuja kuuza hapa Tanzania au sehemu yoyote penye soko la uhakika na salama. Niliwahi kuwa nauza dhahabu kwa mfumo huu mwaka 2014 lakini kwa sasa ofisi hiyo ilifungwa na sina taarifa za wanunuzi wengine wa uhakika na salama kama ile ofisi.
Kwa sasa napenda kujua hasa wanunuzi wa Almasi ghafi (rough diamonds) kwa hapa Tanzania au nje ya Tanzania. Kwakua sasa nimepata soko la uhakika la kununulia na pia kuna watuwa nje ya nchi ambao nao wanapenda kunitumia kuja kuwauzia mzigo wao hapa Tanzania kwani wao wanaamini na wanasema wanazo taarifa kuwa Tanzania kuna bei nzuri na ni salama sana kwa biashara hii. Hivyo ningependa kupata wanunuzi wenye uhakika ili nijenge imani Kwa watu hawa walio amua kuniamini mtanzania mwenzenu, vilevile nami niweze kuwa na uhakika wa kufanya biashara hii na kujikwamua kiuchumi.
Pia kama kuna mwenye wazo lolote la kushauri au kuchukulia tahadhali basi napenda mnielimishe.
Tafadhali naomba mawazo yote yawe hapa wazi ili na wengine wajifuze kwa lolote. Naheshimu kila mchango wa mtu.
Karibuni sana.