Wanyama ndiyo wanaomtibu binadamu.

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
5,184
Reaction score
5,435
Bwana yesu asifiwe na wale wengine asalaam aleykum.
Kila mtu hazuiliwi nini aamini kwa wakati gani na kwanini.

Wapo watu wanaamini yesu atosha hata akiugua hawezi kunywa dawa yoyote anaamini yesu anatosha na kwa kufanya hivyo wanapona kwa kigezo cha imani yao.

Wapo wanaotumia dawa za kisasa tu kwao kutumia dawa za asili wanyama na mitishamba ni dhambi nao kundi hili wanapona kwa kigezo cha imani yao.

Wapo wanaoamini kwa dua za Allah tu na dawa za kisasa na wanapona kwa imani yao.
Wapo wanaotumia dawa za kisasa, za asili, imani ya mtume, imani ya kikristo na zingine zote zitakazoonekana ili mradi tu yeye apone.
Nataka kueleza muujiza wa mnyama mmoja wa porini na jinsi alivyo na uwezo wa kutibu moja ya magonjwa yanayompata binadamu kwa njia za asili.

Elimu kuhusu mnyama huyu nilidodosewa na mhenga ambaye kwa sasa alishatangulia mbele ya haki.
Kuna ugonjwa ambao kitaalamu sijui unaitwaje ila mtu anapoenda kujisaidia mkundu hutokeza nje wote na akishamaliza huanza kurudi taratibu lakini kwa maumivu makali.

Hali hii huwakuta watu wote hasa wenye umri mkubwa wa uzee na umri wa kati. Kiukweli ugonjwa huu unaua pia kama yalivyo magonjwa mengine.
Nirudi kwa mnyama anayehusika na kutibu ugonjwa huu si mwingine bali ni KOBE hapa hata kasa wa bahari aweza kutumika.
Sifa za kobe ni zipi!, mnyama huyu anapoenda kujisaidia jinsi kinyesi chake kitokavyo nje ndivyo utumbo wake mkundu, pull linavyotoka nje pia na akishamaliza haja hulivuta liutumbo tena ndani na hakuna tatizo maana system yake alivyoumbwa hakuna tatizo.

Kutokana na sifa hizo that's why akaonekana mbele ya wajadi wa tiba kuwa ni tiba.
Vifaa vitumikavyo hapa ni maganda ya mkuyu, unyoya wa jogoo, mafuta ya mbarika (castor oil), utumbo wa mkunduni wa kobe.
Vitu hivi huchangangwa na kunuizwa yaani kuviombea ili viwe dawa kwa tatizo husika na mtengeneza dawa hulazimika ajicommit kuwa ana amani na mgonjwa hata ikiwa hataridhika na malipo au vyovyote. Hii ni kama dua sala kwa dawa. Hapa Mungu muumba wa viumbe vyote huhusishwa.
Baada ya hapo dawa hiyo hutumika kwa kushindiliwa sehemu ya nyuma huku mafuta ya nyonyo mbarika yakitumika kama rubricants.
Hii ni today's asili kutumia kobe.
Tuwaheshimu na kuwatunza wanyama wetu kwa afya zetu wenyewe.
 
Huu ni ushirikina kabisa unatuzuga na bwana yesu asifiwe sijui aleikhum nn
Kila dawa ina baraka zake. Siku zote mtu akikutwa na mzizi huitwa mchawi ila mwenye kidonge haitwi mchawi. Tatizo tumepumbazwa na kutokuielewa biblia.
Ndiyo maana leo mzungu akifa anahesabika mtakatifu lakini mwafrika anakuwa jini na kuogopwa hata kaburi lake.
Ungeeleza uchawi ulipo hapo nijifunze kitu. Dua ni dua tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…