Wanyama watano wanaopewa heshima jeshini

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Kwa kawaida wanyama hurahisisha maisha ya binadamu kwa kuwa walinzi, chakula na usafiri lakini kuna baadhi ya wanyama na ndege walioweza kujiwekea heshima duniani hasa kwenye sekta maalum za kijeshi na wameweza kupata nafasi za juu jeshini.

1: SIR NILS OLAV
6890c7e440b3cb9557129cc72666fee6.jpg

Nils Olav ni ndege aina ya Penguin aliyepewa cheo mara ya kwanza mwaka 1972 na kuwekwa kwenye timu ya walinzi wa mfalme Harald V Loudon wa Norway. Kwa sasa Sir Nils Olav ni Brigedia anapewa heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa saluti na kukagua jeshi.

2: TREO
c85ae688e5d4b0ad68a0136658303aa6.jpg

Ni mbwa aliyetumikia jeshi la Uingereza kuanzia mwaka 2001 mpaka 2015. Trio ana medali zisizopungua 63 ambazo alipewa baada ya kufaya kazi kubwa ya kutegua mabomu na kutambua mahali mabomu yalipofichwa.

3: WILLIAM OF ORANGE
f399cc69b235b78642ae2f95565d1a3c.jpg

William ni njiwa aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uingereza mwenye namba MI14 ambapo mwaka 1944 alipewa medali ya 21 baada ya kupeleka ujumbe uliookoa vifo vya zaidi ya wanajeshi 2000 kwenye vita ya Arnhem wakati wa Vita ya Pili ya Dunia.

4: TAFFY IV.
76c256b919e8956ac6088a48b92697f4.jpg

Huyu ni mbuzi aliyetumikia jeshi la Uingereza tangu mwaka 1775 ambaye alichukuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1774 na kuingizwa kwenye jeshi maalum la Uingereza alipokutwa anarandaranda porini. Alipewa medali ya 14 ambayo ni maalum waliyopewa wanajeshi wa Uingereza wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia (WWI).

5: LIN WANG
4de1d332837e2d23dda2f54d413d1391.jpg

Ni tembo aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la China kuanzia mwaka 1942 ambapo alitumika kujenga majengo marefu ya jeshini, kusafirisha chakula wakati wa vita na alitumika kama kivutio kwa ajili ya kukusanya fedha wakati wa njaa kipindi cha vita na kupewa medali 12 za kijeshi.
 
Hao hawana lolote kwa faru wetu fausta na john wanaheshmika balaaa bora uishike sirikali matako kuliko hao viumbe

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app

Lakini, ni ya kweli haya?

Sent from my SM-A300FU using JamiiForums mobile app

Ungetuwekea na wa Tanzania...kwani wapo pia!

Bundi pia anahusika

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app

Hatari sana yana wanyama wanachafuka medali zaidi ya binadamu bana.....afu usisahau kuna paka mmoja alikuwa meya pale marekani.

Kwa kawaida wanyama hurahisisha maisha ya binadamu kwa kuwa walinzi, chakula na usafiri lakini kuna baadhi ya wanyama na ndege walioweza kujiwekea heshima duniani hasa kwenye sekta maalum za kijeshi na wameweza kupata nafasi za juu jeshini.

1: SIR NILS OLAV
6890c7e440b3cb9557129cc72666fee6.jpg

Nils Olav ni ndege aina ya Penguin aliyepewa cheo mara ya kwanza mwaka 1972 na kuwekwa kwenye timu ya walinzi wa mfalme Harald V Loudon wa Norway. Kwa sasa Sir Nils Olav ni Brigedia anapewa heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa saluti na kukagua jeshi.

2: TREO
c85ae688e5d4b0ad68a0136658303aa6.jpg

Ni mbwa aliyetumikia jeshi la Uingereza kuanzia mwaka 2001 mpaka 2015. Trio ana medali zisizopungua 63 ambazo alipewa baada ya kufaya kazi kubwa ya kutegua mabomu na kutambua mahali mabomu yalipofichwa.

3: WILLIAM OF ORANGE
f399cc69b235b78642ae2f95565d1a3c.jpg

William ni njiwa aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uingereza mwenye namba MI14 ambapo mwaka 1944 alipewa medali ya 21 baada ya kupeleka ujumbe uliookoa vifo vya zaidi ya wanajeshi 2000 kwenye vita ya Arnhem wakati wa Vita ya Pili ya Dunia.

4: TAFFY IV.
76c256b919e8956ac6088a48b92697f4.jpg

Huyu ni mbuzi aliyetumikia jeshi la Uingereza tangu mwaka 1775 ambaye alichukuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1774 na kuingizwa kwenye jeshi maalum la Uingereza alipokutwa anarandaranda porini. Alipewa medali ya 14 ambayo ni maalum waliyopewa wanajeshi wa Uingereza wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia (WWI).

5: LIN WANG
4de1d332837e2d23dda2f54d413d1391.jpg

Ni tembo aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la China kuanzia mwaka 1942 ambapo alitumika kujenga majengo marefu ya jeshini, kusafirisha chakula wakati wa vita na alitumika kama kivutio kwa ajili ya kukusanya fedha wakati wa njaa kipindi cha vita na kupewa medali 12 za kijeshi.
Kuna wakati hii taaluma ya kijeshi huonekana kama vichaa. Brigedia kwa mnyama?
 
Bongo njaa kali jeshi linafuga njiwa wa kutuma ujumbe mara wanashangaa anakonda tu kumbe kuna wanajeshi wanaiba mtama wanaenda kuuza.
Au wanakula wenyewe, hawataki shida kabisa

Na huyo mbwa biskuti zake wanapelekewa watoto
 
Back
Top Bottom