Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
WANYASA WANAULIZA DENIS PHOMBEAH NI NANI KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA ?
Raia Mwema 14 - 20 Agosti, 2019
Raia Mwema la 14 - 20 Agosti limechapa makala ambayo kwanza ilikuwapo hapa Majlis, ''Tulikotoka Kufika SADC Kisa Cha Ally Sykes, Denis Phombeah na Kenneth Kaunda.''
Nia yangu ya kuweka hapa makala ile ilikuwa baada ya kupigiwa simu na kuombwa nishiriki katika kipindi cha Channel Ten Zahir Hotel ambako wajumbe wa SADC wangefika pale na kuniuliza maswali kuhusu historia ya mgahawa huu na wapigania uhuru wa nchi za Kusini.
Kwenye mlango wa kuingia mgahawa huu kuna kibao kinachoeleza kuwa hapo palikuwa sehemu wakikutana wapigania uhuru wakati wa nchi Kusini ya Afrika.
Kipindi hiki nilifahamishwa kitarushwa mubashara.
Ukweli nilimkatalia huyo aliyenipigia simu na sababu kubwa ni kuwa mwaliko wenyewe umenifikia mchana milango ya saa saba hivi na kipindi kinakwenda hewani saa kumi jioni kwa hiyo hapakuwa na muda wa matayarisho.
Mambo kama haya yanahitaji maandalizi hasa ikiwa kipindi ni mubashara kwa kuchukua tahadhari kusema maneno siyo.
Nikamfahamisha hilo ndugu yangu aliyenifikishia mwaliko nikamwambia hawa ni wageni wa serikali wasije wakaniuliza maswali ambayo majibu yake yanapishana na historia rasmi inayofahamika.
Ikawa nimekataa kushiriki katika kipindi kile.
Lakini ikanijia fikra kuwa ninao bado mchango wa kuchangia katika historia ya Tanganyika na SADC.
Ndiyo nikaamua kuweka hapa safari ya mwaka wa 1953 ya Ally Sykes na Denis Phombeah kwenda Lusaka Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa kutoka nchi Kusini ya Sahara ulioitishwa na Kenneth Kaunda akiwa Rais wa ANC ya Northern Rhodesia.
Ndugu zetu Wanyasa baada ya kusoma gazeti la Raia Mwema na kukuta Mnyasa anaiwakilisha Tanganyiaka katika mkutano ule wamepiga simu nyingi Raia Mwema kutaka kujua mchango wao katika uhuru wa Tanganyika.
Kisa hiki hiki kilichosomwa na wengi hapa Majlis kama ningekieleza mbele ya camera za televisheni tena mubashara athari yake kwa watazamaji ingekuwa nyingine kabisa.
Lingeweza kuja swali kwangu, ''Ally Sykes na Denis Phombeah ni nani na iweje hawa wawakilishe Tanganyika kwani Julius Nyerere alikuwa wapi?''
Unajibu vipi mtu maswali kama haya?
Mhariri wa Rais Mwema kakwepa kuliunganisha jina la Ally Sykes, Denis Phombeah na jina la Kenneth Kaunda.
Si bure kwa yeye kuamua kufanya hivi.
Anazo sababu zake.
Picha: Ally Sykes na Denis Phombeah wakiwa Chileka Airport, Blantyre Nyasaland wakiwa njiani kurudi Dar es Salaam.