Wanyaturu wamemkosea nini huyu DJ anayetafsiri filamu na series za nje? Haoni kama anatengeneza chuki ya ukabila?

Wanyaturu wamemkosea nini huyu DJ anayetafsiri filamu na series za nje? Haoni kama anatengeneza chuki ya ukabila?

Darucha

Senior Member
Joined
Dec 28, 2020
Posts
111
Reaction score
211
Huyu DJ mtafsiri wa movies na series za nje anawaponda sana Wanyaturu sijui wamemkosea Nini kwa kweli anaudhi sana huyu. Kila kitu yeye ni Wanyaturu, Wanyaturu mpaka Kero yaaani. Wanyaturu kamshtakini huyu kwa kuwafanya muonekane watu wa Karne ya 20.

Hizi ni baadhi ya kauli zake anazozitoa pindi anapotafsiri movie zake:

1- Bora wanyaturu Mia sita wafe kuliko wazungu wawili maana wanyaturu hawana msaada kwenye Karne hii
2- Watu kumi na wanyaturu wawili almanusra wapate ajali pale Ngaramtoni
3- Ukikuta Mnyaturu kavaa suti lazima uwe na maswali ya kujiuliza "ina maana suti zimeshuka hadhi siku hizi kila mtu anajivalia tu?"

Sio kauli hizi tu, ana kauli nyingine huyu.
 
Mkuu jamaa anapenda tu utani na ukizingatia pia wanyaturu ni watani wake, nje ya maada kidogo: Jamaa yuko vizuri ndo dj pekee (ommy dj) anaenishawishi kuangalia muvi na series za kizungu zilizotafsiriwa anajua kingereza na ana content balaa, sio hawa madj wengine full makelele plus kutafsiri uongo. Thank you mleta maada.
 
Jasmoni Tegga,

Mzee keshakufa. Mada ya juu, kwanini mtafsiri was tamthilia na senema za kizungu anakashifu kabila za watu?

Turudi huko sister.
 
Back
Top Bottom