Wanyonge tuunganishe nguvu kumuokoa Diamond

Alivyokua anaimba jana alikua anazomewa vibaya sana.... watu wanamshabikia Ali kiba huku Diamond yuko stejini

Anasema watu wangu wa kinondoni vipi watu Booooo.. ndio hujuma inaongelewa hiyo..

Duu.hiyo ni dalili mbaya hata akiamua kuipotezea.Aangalie alipokosea arekebishe.Kiba naye aliimba?hakuzomewa na team domo?
 
Ukishindwana na middleman,CV anaitia shombo.

Hata aki-focus kwenye media za nje zaidi kama hapati support ya ndani ni sawa na bure.

Cha muhimu ajue chanzo cha tatizo na aweke mambo sawa la sivyo,zitabaki story.
 
Kazi nzur Diamond umeifanya tz na bongo fleva kufahamika kimataifa kwa sababu miaka mitatu au minne iliyopita tz tulikuwa tunakimbizwa na jirani zetu Kenya na Uganda kupitia video lakini uthubutu wako umeifanya tz kuwaacha mbali sana hao jamaa vile vile umeamsha hali hata kwa video producers /directors wa hapa nyumban kutoa kazi zilizosimama....piga kazi kijana penye riziki hapakosi fitina coz hizo kelele za wahuni wachache najua ni wivu tu kuona kijana mwenzao unasumbua mjini mpaka nje ya tz...uzuri ni kuwa wewe jamaa( Diamond) unajitambua sanaa sio kama wasanii wengi wa kibongo wanaopenda kulewa sifa...good job Diamond....
 
Duu.hiyo ni dalili mbaya hata akiamua kuipotezea.Aangalie alipokosea arekebishe.Kiba naye aliimba?hakuzomewa na team domo?

Kiba aliimba... ye hakuzomewa hata kidogo alikua anashangiliwa mwanzo mwisho.... nadhani hata yeye zile shangwe hakuzitegemea..

Diamond arekebishe hizo dharau wanasema anazo otherwise nae ni msanii mzuri sana
 
Ukishindwana na middleman,CV anaitia shombo.

Hata aki-focus kwenye media za nje zaidi kama hapati support ya ndani ni sawa na bure.

Cha muhimu ajue chanzo cha tatizo na aweke mambo sawa la sivyo,zitabaki story.


apunguze dharau,na ninacho kiona siku akishuka kimziki atakuwa kama Mr. Nice . hata kuwa kama Juma Kiroboto
 
Menejiment yake iangalie upya jinsi yeye almasi anabyofanya kazi zake. Wakuinua kazi zake ni menejiment yake na wao ndio wanaweza kumuangusha.

Kuna vitu mtu anaongea vinaweza kuathiri utendaji wa kazi zake, hasa hawa masupastaa na wanasiasa. Ndio maana wengi huajiri watu wa kuangalia mienendo yao hasa kwenye mitandao ya kijamii., mahojiano na waandishi wa habari na majibizano na wasanii wenzake ambayo kwa hakika hayana tija kwenye kazi zake. Awe na watu wanaomskrutini na kumkanya yapi aseme na yapi asiseme au kujibizana na mtu. Bahati mbaya Mimi sio shabiki wa mziki, hata ukiniuliza ana nyimbo ngapi mwaka huu sina weledi, lakini mtukama almasi ni kioo cha Tanzania na hatuna budi kuinua kipaji chake na kumpa sapoti. Haijalishi wewe ni shabiki wake ama la. Kuna yule dogo alikuwa akija sana jf heaven on desert, huu ndo wakati wa kufanya kazi ili kuhakikisha chati ya almasi inabaki juu. Tatizo letu watanzania ni wivu. Tunataka wote tuwe masikini.
 
Last edited by a moderator:

sawa hata mwaka mmoja nyuma p square walikuwa top Nigeria ila sasa hivi ni Davido
Maisha ndivyo yalivyo kama ukiwadharau waliokupandisha na kukushusha itakuwa rahisi
kubomoa ni rahisi kuliko kujenga
hawezi kusema mbeya hakuna hotel ya hadhi yake wakati miaka mitano nyuma alikuwa akiishi tandale
yuko wapi Mr nice ? Huyu ndie aliringa kupanda jukwaani akiwa back stage na chameleon akapanda akaimba
Hakuna wa kudumu milele ingekuwa yupo maisha yangeboa sana
 
diamond hajijua bado anaamini kupgiwa magoti mbele yake n fahari.hatukatai he is reach far in music.lakn s bora kuna watu wanaweza kuimba kulikon yeye na wanapendwa sana.usionyeshe dharau kwa walioko chn kama unavyodhan.ur best lnk with best.sio kusema kwa over confdence like m nipo juu xana walianza xjui bele,sam wa ukwel,kasm xjui tid xjui omy xaxa kiba.hata mesi akihojiwa juu ya ronaldo anampa heshma zake na ronaldo pia.ali anamuongelea poa diamond.
 
Alivyokua anaimba jana alikua anazomewa vibaya sana.... watu wanamshabikia Ali kiba huku Diamond yuko stejini

Anasema watu wangu wa kinondoni vipi watu Booooo.. ndio hujuma inaongelewa hiyo..


Kama hiyo ndo hujuma, kuna mtu/kundi la watu liliendesha kampeni kuwa azomewe? Na kama cloud ya watu ilizomea, yeye hawezi kuona sehemu fulani kalegea?

Anyway, katika issue yoyote ile, ups and downs zipo sana tu!
 
Kiba aliimba... ye hakuzomewa hata kidogo alikua anashangiliwa mwanzo mwisho.... nadhani hata yeye zile shangwe hakuzitegemea..

Diamond arekebishe hizo dharau wanasema anazo otherwise nae ni msanii mzuri sana

Kama ana masikio atasikia na kujirekebisha.Nadhani bado ana akili za kitoto.Nani kati yao alitangulia kupanda jukwaani!?
 

kuna wakati mapungufu yanazid sasa na kuwa upuuz
 
Si mpenzi sana wa nyimbo za bongoflava lakin ALIKIBA namkubal nyimbo zake!!! Toka enzi za cindelela ...macmuga...dushelele...na mpaka kesho...kiba anaweza...!! Kaza buti usiwe na dharau na majivuno kama akina naniii!!! Viva kiba!!
 
Domo ni.msanii mzuri

Tatizo lake anapenda kupaishwa kwa scandal ( ndio mbinu yake ya kubakia kwenye vyombo vya habari na midomoni mwa watu) sasa mbinu yake hii inamkosti



Kiba aliimba... ye hakuzomewa hata kidogo alikua anashangiliwa mwanzo mwisho.... nadhani hata yeye zile shangwe hakuzitegemea..

Diamond arekebishe hizo dharau wanasema anazo otherwise nae ni msanii mzuri sana
 
Kama ana masikio atasikia na kujirekebisha.Nadhani bado ana akili za kitoto.Nani kati yao alitangulia kupanda jukwaani!?

Swali lako ni la msingi sana. Iliwahi kusemwa kuwa maisha haya ni mafupi na unatakiwa kuchunga sana ndimi na matendo yako pia. Mr. Nice naamini hadi sasa kwa hawa Bongo flavor naamini hata hawa Bongo Movie hakuna hata mmoja amewahi kutunisha Account ikasoma 1bn/-, lakini leo hali yake kiuchumi sote tunaijua. Kuna wakati tahadhari hiyo ilitolewa fans wa Almasi wakasema huyo Almas yuko makini, wanachopaswa kujua ni kuwa hata matajiri wakubwa huporomoka pia.

Hivyo Almasi asije akajisahau sana kwenye haya maisha, chochote kinaweza kutokea, na ikifika hivyo itabidi tu ukubaliane na hali hiyo, no way out.
 
HUU HAPA UTHIBITISHO.Mali ni nyingi nyumbani, kipi kimekukimbiza,Hapa Alikiba, anamwambia Diamond, nyumbani ( SHAROBARO RECORDS) kuna kila kitu, beats kali, management nzuri and all that, kitu gani kilimkimbiza SHAROBARO RECORDS?Ona babio mamio wote wanakulilia,HAPA ALIKIBA ANAMAANISHA, SHAROBARO RECORDS, WAKIONGOZWA NA BOB JUNIOR, WOTE WANAMLALAMIKIA DIAMOND KWA KITENDO CHAKE CHA KUKIMBIA KUFANYA KAZI SHAROBARO. (BOB JUNIOR ALIPIGA KELELE SANA DIAMOND ALIPOKIMBIA SHAROBARO RECORDS )Mtoto pekee ako nyumbani, kipi kimekukimbiza,HAPA ALIKIBA ANASEMA, DIAMOND ALIKUWA NDO ARTIST PEKEE MKALI ALIYEKUWA CHINI YA SHAROBARO RECORDS. HAKUKUWA NA UPINZANI WOWOTE NDANI YA SHAROBARO, KITU GANI KILIMFANYA AONDOKE ?Ona babio mamio wote wanakuliliaNdani ya Dar es salame ulikuja bureHAPA ALIKIBA ANAMKUMBUSHA DIAMOND, KUWA SIKU ALIPOKWENDA SHAROBARO RECORDS KWA MARA YA KWANZA, HAKUWA NA HATA SENTI TANO NA ALIREKODIWA WIMBO WAKE BURE KABISA.NENO DAR ES SALAME, LIMETUMIKA KUMAANISHA SHAROBARO RECORDS AU MUSIC INDUSTRY.(KAMA ULIKUKUWA HUJUI, ALIKIBA NI MMOJA KATI YA WANAHISA WA SHAROBARO RECORDS, NA NDIO ALITOA IDHINI KWA BOB JUNIOR, AREKODI BURE WIMBO WA DIAMOND. ILIKUWA HIVI DIAMOND ALIENDA KWA BOB JUNIOR NA KUMWAMBIA ANA WIMBO WAKE ANAOMBA UREKODIWE LAKINI HANA UWEZO WA KIFEDHA, BOB JUNIOR AKAOMBA KUMSIKILIZA, ALIPOMSIKILIZA AKAGUNDUA KIPAJI CHA DOGO, BUT HAKUWA NA MAMLAKA YA KUREKODI WIMBO HUO BURE BILA IDHINI YA BOSS, ALIKIBA, SO IKABIDI AENDE KWANZA KUOMBA IDHINI KWA ALIKIBA, ALIKIBA AKAMWAMBIA BOB JUNIOR KAMA DOGO ANAJUA KUIMBA VIZURI, MREKODIE TU, HAKUNA SHIDA. ALIKIBA ALIYASEMA HAYA AKIWA ANAYAFANYA MAHOJIANO KWENYE KIPINDI CHA MKASI HIVI KARIBUNI.Tena kimwana, kimwana hujui kuchuna WAKATI DIAMOND, ANAENDA KUOMBA KUREKODI KWA BOB JUNIOR, ALIKUWA TAYARI KUFANYA SHOW ZAKE HATA BURE ILIMRADI TU AWEZE KUJITANGAZA..DIAMOND ALIWAHI KUMUOMBA ALIKIBA, APANDE NAYE KWENYE SHOW YA ALIKIBA, BILA MALIPO YOYOTE ILI WATU WAMUONE AKIWA NA ALI KIBA. SO ALIKIBA AMETUMIA NENO “KIMWANA ASIYE JUA KUCHUNA” AKIMAANISHA ‘MSANII UNDERGROUND ALIYE TAYARI KUIMBA HATA BILA MALIPO.Na zile lawama za wale walokuzoeza,HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA LAWAMA ZA MADEMU WANAO TOSWA NA DIAMONDUlikuja jana na leo tofauti sana.HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA NAMNA AMBAVYO DIAMOND AMEBADILIKA KITABIA BAADA YA KUPATA MAFANIKIO KIMUZIKI.Tena bora Yule wa jana, wa leo tofauti sana,HAPA ALIKIBA ANAWAZUNGUMZIA WEMA SEPETU NA PENNY, ANASEMA BORA HATA PENNY KULIKO WEMA AMBAYE NDIO YUPO NA DIAMOND KWA SASADakika mbili mbele nyuma, kichwa kinaumaHAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA TABIA TABIA ZA WEMA SEPETU. MKOROFI(DAKIKA MBILI MBELE NYUMA), NA MWINGI WA HABARI, AMA PASUA KICHWA ( KICHWA KINAUMA) AMA KICHECHE.Tena bora Yule wa jana, wa jana leo wa jana,HAPA ALIKIBA ANASISITIZA ANACHO KIMAANISHA, KWAMBA ANAMZUNGUMZIA WEMA, ” tena bora yule wa jana, wa jana leo wa jana ” YANI YULE AMBAYE UPO NAE LEO, NA AMBAYE ULIWAHI KUWA NAE ZAMANI. NI WA JANA, UPO NAE LEO, LAKINI ULIWAHI KUWA NAYE JANA. HUYO NI WEMA SEPETU, ALIWAHI KUWA NA DIAMOND, WAKAACHANA, WAMERUDIANA TENA. ( ‘WAJANA LEO WA JANA = WEMA SEPETU )Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinaumaHAPA ALIKIBA ANAKUTOLEA UFAFANUZI ZAIDI KWAMBA, HUYU ” WA JANA LEO WA JANA” SI MWINGINE ILA NI WEMA SEPETU. ANAFANYA HIVYO KWA KUELEZEA TABIA YA WEMA SEPETU AMBAZO NI “UKOROFI” (DAKIKA MBILI MBELE NYUMA ), NA UKICHECHE A.K.A PASUA KICHWA (KICHWA KINAUMA)..KAMA UMESAHAU WEMA SEPETU ALIWAHI KUMTUKANA BOB JUNIOR MATUSI YA NGUONI, KESI IKAENDA MAHAKAMANI..UNAKUMBUKA HIYO?Oyayee , mbona unawatesa sana,HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND MBONA UNAWATESA SANA HAO WASICHANA UNAO WABADILISHA BADILISHA ?Omamee, omame oya mame, omame oya mameeMbona unajitesa sanaHAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND “WHAT GOES AROUND COMES AROUND”. ANAVYO WATESA HAO WSICHANA, NI SAWA NA KUJITESA MWENYEWE TU. UKICHECHE WA DIAMOND UNAMTESA KIASI CHA KUMFANYA ASHINDWE KUJUA AMPENDE NANI KATIKA MAISHA YAKE, KWA SABABU WANAWAKE KARIBU WOTE ANAO TOKA WANAKUWA NA KASORO ZISIZO VUMILIKA.Omamee, oya mame, omame oya mameeUkaanza kulewa , madawa kuvuta kwa sana.HAPA ALIKIBA ANATHIBITISHA NAMNA AMBAVYO HALI YA KUWATE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…