‘Wanywa pombe kali hatarini kupata upofu’

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



KWA UFUPI


  • Mbali na unywaji pombe, pia kuvaa miwani ya urembo au ya kusomea bila kupata ushauri wa daktari, ni miongoni mwa sababu za kupunguza uwezo wa macho kuona.



Dar es Salaam. Unywaji pombe kali kupita kiasi, umetajwa kuwa chanzo cha upofu, huku uhaba wa madaktari wanaotibu ugonjwa huo, vifaa tiba vikielezwa kuwa kikwazo.

Mbali na unywaji pombe, pia kuvaa miwani ya urembo au ya kusomea bila kupata ushauri wa daktari, ni miongoni mwa sababu za kupunguza uwezo wa macho kuona.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando wakati akipokea kompyuta mpakato 34 zenye thamani ya Sh46 milioni, zilizotolewa na Shirika la Sight Savers kwa ajili ya kukusanya takwimu za ugonjwa huo kwa mikoa saba jana Dar es Salaam.

Dk Mmbando alisema ugonjwa wa macho unachangiwa na vitu vingi, lakini matumizi ya vitu bila ushauri, ikiwamo unywaji wa pombe kupita kiasi kuvaa miwani bila kupata maelekezo ya kitabibu vinachangia.

"Watu wengi wananunua miwani ya kuongeza uwezo wa kuona na urembo bila kupata maelekezo, wengi wao hawafahamu kuwa hata miwani ya urembo ni lazima kuvaa kwa kufuata maelezo ya kitabibu," alisema Dk Mmbando.

Dk Mmbando alizitaka halmashauri za mikoa ya Mbeya, Rukwa, Kigoma, Tabora, Morogoro, Iringa na Manyara kuingiza vitendea kazi hivyo katika orodha ya vifaa vya hospitali na kuhakikisha vinatumia kwa kazi iliyokusudiwa.

Mratibu wa wizara hiyo, Dk Nkundwe Mwakyusa alisema uhaba wa madaktari ni kikwazo katika kutoa huduma ya matibabu ya macho nchini.

Alisema madaktari bingwa wa macho nchi nzima idadi yao ni 40, ambao kimsingi hawatoshelezi mahitaji ya wananchi.

Mkurugenzi wa Fedha na huduma kutoka Shirika la Sight Savers Andrew Kilewela alisema wameamua kutoka kompyuta hizo ili kuimarisha uratibu wa huduma za afya ya macho.chanzo.www.mwananchi.co.tz
 

Attachments

  • Mtambo-wa-kutengeneza-pombe-aina-ya-gongo.jpg
    28.6 KB · Views: 190
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…