Wapaka mbao rangi kuhadaa wateja

Kuna jamaa yangu ni fundi,amenishauri mbao nyingi kwa sasa hamna kitu.

Anasema kitu cha uhakika ni milunda,ambao mmetumia naomba uzoefu kuhusu hili
Milunda ni imara sana.
 
Oil chafu haisaidii, nakusanua mapema sana
Inasaidia sana tu. Mchwa, sisimizi, hawapatani na harufu ya oil chafu. Hakikisha hii kwa kuipaka sehemu walipo hao wadudu watahama ndani ya masaa machache.
 
ni bora kujifunga mkanda kununua sao hill wao treated timber zao huwa ni uhakika.
Na hapa ni Kujifunga Mkanda haswa, ila unapata Kitu cha Uhakika, Mimi nilienda kuulizia, wanakwambia kabisa, Mbao mnazo nunua ni hazina dawa, Mbao haziwekwi dawa kwa kuchovya.
Ila tuu Bei ya Sao Hill ni ya Moto, lakini nadhani itakusaidia kuepusha hasara siku za Usoni.

Nyumbani kwetu wiki iliyopita, Gypsum ya Sebuleni imedondoka, Kuanzia Mbao zile za Blandering na Kenchi zote zimeliwa, Na nyumba ina miaka kama 15 tangu imejengwa.
 
Ninachofahamu kuna mbao tunaita 'treated'. Hizi hua ndefu sana na huuzwa kwa kupimwa urefu wake, bei ni kwa kila 'futi'. Hizi ndio hutiwa dawa kiwandani, na hazina wateja sana kutokana na bei yake.

Kuna hizi nyingine zina urefu wa 12ft, hizi ndio tunatumia sana mitaani. Hizi hupakwa dawa na wauzaji. Unanunua Lita 20 ya dawa unachanganya na maji mengi tu (inaruhusiwa) kisha unapaka au kuloweka hizo mbao. Utiaji wa dawa wa namna hii haudumu sana kama ambavyo itadumu mbao iliokuwa 'treated' kiwandani.

Kuchanganya dawa na rangi ya ukindu ni kumuwezesha mteja kutofautisha mbao ipi ina dawa na ipi haina dawa.
Utiaji wa dawa wa aina ya pili unaweza kufanya hata site kwako kabla hujazitumia, ni simple tu, ukiwa na vijana wawili ni kiasi cha 'lisaa limoja' Kwa mbao zote za kutosha kuezekea nyumba yako.

NOTE;
Mbao iliowekwa dawa haitokaa milele isioze, Ila inategemea na uwiano wa mchanganyo wa dawa na maji, pia hiyo mbao imenyonya dawa Kwa muda gani na aina ipi ya dawa.

Samahani mie ni fundi tu, naongea Kwa experience kwa jinsi tunavyokutana navyo mitaani.
 
Mbona kijijini tunajenga nyumba tena za makuti na zinakaa 15 to 20 yrs? Kwani lazma Dawa?
 
Nimesoma huu uzi nimejua kabisa hapo Buguruni washanitia kidole sasa sijui nikaezua paa nipakie dawa juu kwa juu au niache tu😆
 
Kuna dawa ya kupuliza, nitaulizia jina lake. Unachangaya na maji unaweza kwenye ile bomba ya kupulizia....haimalizi tatizo ila angalau italipunguza.
Ngoja na mimi nikapulize tu maana nishapigwa.

Lakini sasa ningejuaje?
 
Wale madactari wa ujenzi hawapo humu watupe suruhisho maana miaka mitatu udsm sio mchezo
 
Kumbe ni nini?
Wale ni beetles .....ulishawahi kula embe na kupasua lile kokwa lake? Kama uliwahi bila shaka ulikutana na yule funza au mdudu flani mweusi. Je ulijiuliza kaingiaje? Ni kweli ulijiuliza ila jibu hukupata.
Yale ni mayai yanatagwa kwenye ncha za majani ya mti wakati unachanua kwenye harakati za ukuwaji, hvo hayo mayai yanakuwemo ndani ya mti mpaka pale unachanwa mbao, kosa ni pale mti huo unapokauka ndo hayo mayai hufufuka na kuanza kuutafuna huo ubao. Hayo mayai inasemekana yanaweza kudumu kwenye ubao miaka zaidi ya 48.
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…