wapambe wa Mama sasa ni kumsherehesha na kumsifia tu. Mambo muhimu hawajali. Waziri anapata shida kwenda kuongea na Mama sera za elimu lakini kila siku ni Mama ni kushsreheshwa au kusifiwa tu. Mara tuzo, mara matamasha , mara kachaguliwa kweli hili, mara birthday. Waziri wa elimu kapewa kwa shida masaa mawili tu atoe muelekeo na sera ya elimu ya watoto wetu. Hawa wapambe hawajali vitu muhimu. Wanajeshi wamekufa Mama haja hutubia taifa kama amiri jeshi mkuu. Bendera sio nusu. Ni sherere sherehe kila siku. Misaada ya dawa kutoka USAID imesitishwa hatuambiwi itakuwaje inawezekana hata waziri hampati Mama yuko busy anafikiria kwenda kucheka na Baba levo Dodoma. Mimi nashauri Tuombee hii nchi. Huyu Mama wetu kama walivyosema Mbowe kabla ya kwenda gerezani alikuwa mtu tofauti. Mama huyu sio yule wa 2021-2022