Wapangaji wenzangu, mnakabiliana vipi na jirani asiyetaka kulipia bili ya maji na umeme?

Hao wakorofi mi nawapenda sana.
Chomoa waya 1 tu wa Neutral unaoelekea kwake.
Bomba anza ukarabati uelekeo kwako kisha lifunge
 
Nadhani ni matumizi, Kuna kiwango ukivuka umeme unalipia tofauti na watu wengin. Kupandishwa grade same unit unazonunua kwa 10k mtu mwingine anapata zaidi ya hizo.
Kumbee!! Basi umeme wangu haukai aisee elfu10 napata unit 28 lakini kila wiki mbili lazima ninunue😩
 
Kabisa mkuu....umenena vyema
 
Mimi nilikuwa na wapangaji dizaini ya hela ya bill hadi akumbushwe.... sasaivi maji wanauziwa kwa ndoo,huna mia hamsini ya ndoo ya maji,kunywa mikojo yako!
Umeme kwenye mkataba kuna kipengele ukisumbua kulipa umeme tunadisconecti na baada ya hapo utakuwa umevunja mkataba wakuendelea kukaa kwenye nyumba......unakuta mtu tarehe yakulipa maji imefika,hadi mkumbushane,mara anakupiga chenga... Haswa wapangaji hawa vijana.....kwangu sasaivi nataka wapangaji wadada tu maana mostly sio wasumbufu sana
 
Para ya kwanza haiwezi kuwa suluhisho, maana wahusika wanaokeana sio waelewa.

Umeshauri vizuri sana.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hao wakorofi mi nawapenda sana.
Chomoa waya 1 tu wa Neutral unaoelekea kwake.
Bomba anza ukarabati uelekeo kwako kisha lifunge
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sema ukiwa na kipato,ni vyema ukapanga kwenye nyumba za aina fulani..ni zile nyumba zinazo jitegemea unaishi peke ako...ama kwenye hizi apartment za kisasa..ni nadra sana kuishi na watu wa hovyo hovyo kwenye hizo nyumba

Kikawaida ukiwa na maisha ya chini mara nyingi kuwa mtu wa hovyo ni pie.
Huyo jirani angekuwa na pesa hiyo Bills Ange clear tuu.

So hata huko kwenye apartment za wenye pesa kinachofanya uone sio wahovyo ni pesa walizonazo sio vinginevyo. Yaani haihusiani na tabia
 
Nikajua kashindwa kulipa pango sasa Msilaumiane wenyewe kaeni pamoja anzen kumlaumu samia uzur ww ume sgn in jf mwambie akupe point za kumnanga samia mana hapo serikal ndio inawagombanisha umeme ni wa serikal maji ni ya selikali
 
Ingekuwa umeme sawa.

Lakini maji inabidi awe analipia..

Mimi nilikaa na mpangaji mwenzangu hana tv wala friji na sikuwahi kumdai pesa ya umeme.

Mambo mengi tumia ustaarabu tu maisha yasonge kwa amani.
 
Nyumba za kupanga za Kiswahili ugomvi mkubwa ni kwenye bills na usafi.
 
Sisi haya unayotuambia HAYATUHUSU.

Suluhisho mshirikishe mwenye nyumba aliyewapangisha.
 
Katika watu wanapishana na mamilioni ya pesa ni dawasco na tanesco.

Inatakiwa kila mpangaji kuhudumiwa na Shirika moja kwa moja.

Sio shirika kupeleka umeme, maji kwenye nyumba, halafu eti wakaazi ndio waanze kupangiana matumizi.

Kila mpangaji anatakiwa kuwekewa umeme na maji moja kwa moja kutoka tanesco na dawasco.

Namba ya nyumba inakua moja lakini inakua na vipengele vya a, b , c (kulingana na idadi ya vyumba/wapangaji.

Mie naona mapato yatakua makubwa kama haya mashirika yakifanya mfumo huo.

Wajifunze kutoka makampuni ya simu, siku hizi hakuna centre ya watu kwenda kupiga simu, kila mtu ana tambo lake, ufikiwaji umekuq rahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…