Mapengo 17
R I P
- Mar 28, 2014
- 1,229
- 610
WASHIRIKI wa mdahalo wa MkikiMkiki 2015 unaofanyika kila Jumapili mchana na kurushwa na kurshwa na Kituo Cha Televisheni cha Star TV ukilenga kujua sera za vyama kwenye masuala mbalimbali ikiwemo ya Afya na Elimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, wamesema vyama vyao vitasimamia kikamilifu ilani za vyama vyao ili kutekeleza ahadi walizoahidi.
Baadhi ya washiriki wa mdahalo huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam, wengi wao ni wagombea ubunge ukiachilia mbali wale wanaowania nafasi ya urais.
Wakati wa kutetea ilani za vyama vyao wengi wao wameonekana wanapata wakati mgumu wa kutetea ilani za vyama vyao kutokana na sababu mbalimbali.
Mmoja wa washiriki wa mdahalo huo ni Dk. Hamis Kigwangala (CCM) ambaye pia ni mgombea ubunge jimbo la Nzega Mjini kupitia CCM katika mdahalo uliofanyika Oktoba 13, 2015 jijini humo,
Alitetea jinsi serikali ya chama chake na jinsi kinavyoshughulikia sekta hizo sekta za elimu na afya kwa kila mtanzania na kusema kuwa tangu awali chama hicho kimekuwa mstari wa mbele katika kuboresha sekta za afya na elimu.
Alianza kupata wakati mgumu baada ya kuzungumzia mkakati wa CCM kuondoa tatizo la msongamano wa wagonjwa katika hospitali za serikali ambapo ilielezwa kuwa hali ilivyo sasa, kitanda kimoja kinalaza wagonjwa watatu huku kina mama wajawazito wakilala sakafuni alianza kupuuza madai hayo akisema kuwa ni kauli za kisiasa, hivyo kuwataka wananchi wazungumze mambo yenye uhalisia.
Soma zaidi =>Wapata wakati mgumu kutetea Sera za vyama vyao kuhusu Sekta za Afya na Elimu