Wapenda Soka Tanzania hatumdai Eng Hersi Ally Said Rais wa Yanga

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Nianze kwa mfano huu ninapoishi kuna mti wa mwembe watoto hawakauki kwenye huu mti wakitungua maembe, siku moja nikamuuliza mtoto mmoja kwanini mnapenda sana maembe ya huu mti.

Jibu lake Baba haya maembe yako ni matamu sana kushinda miti yote ya mtaa huu nikakumbuka ile kauli” MTI WENYE MATUNDA NDIO UNAPIGWA MAWE”

Twende kwenye mada kwa mpenda soka yeyote yule Tanzania sidhani kama kuna kitu anamdai Rais wa Yanga kwa Sasa Ndg Eng Hersi Ally Said huyu mwamba yale mambo magumu ambayo wengi tunayaona kama ndoto yeye ndiye anayafanya sasa.

Narudia tena ukiaacha wivu, roho mbaya, Ushirikina, majungu, kuharibiana, tamaa mbaya...nk kutoka kwa wachache wetu hakika wanayanga na Watanzania kwa ujumla Injinia ana mengi mazuri japo kama binadamu hakosi mapungufu.

Kuanzia yupo pale Gsm kama Mkurugenzi mtendaji na mdhamini wa Yanga aliutendea makubwa mpira wetu nani angejua Shibobo Style kutoka kwa Morrison kama sio mikono ya Injinia, nani angemfahamu Ticha Mukoko Tunombe, nani angemfahamu Saido Ntibanzokiza.

Nani alitegemea Yanga watamfanya mchakato wa mabadiliko kwa amani kabisa na kupita hatua zote ngumu na mwisho leo Yanga ikiwa timu ya mfano kwa kuendeshwa kisasa.

Kama rais Yanga kuna sajili wana Yanga walikua wanaona kama ndoto ila mwamba anakauli yake “TUKIMTAKA MCHEZAJI YEYOTE YULE HATUMKOSI” leo wengi wanaona kama mazingaombwe Mayele, Bangala, Moloko, Dr Aucho mido, Bangala, Mwamnyeto, Aziz K na sasa Musonda kukipiga pale Yanga.

Eng Hersi Said Ally alifanya maamuzi magumu kwa maslahi ya Yanga kwa kuvunja mikataba karibia ya wachezaji wote na kuanza Upya, hakuogopa bali alifahamu anachokifanya leo tunashuhudia Yanga Tamu ikitoa burudani safi kabisa kwa Soka la kitabuni chini ya Kocha Pro Nabi mtaalamu.

Bila kuangalia blaa blaa Gsm Chini ya Eng Hersi Said walitaka kufadhili ligi yetu kama pacha ndio pale nikasema roho mbaya wa Watanzania wakampiga vita wakiongozwa na Viongozi wa timu ya Simba na Gsm kuamua kuachia ngazi/hatamu.

Kama mwembe mzuri tu lazima utapigwa mawe kwa sasa vimeibuka vikundi vya hawa wanaojiita wachambuzi uchwara wanaojifanya wanafahamu kila kitu na kuacha kujadili mpira kwa kuendekeza pesa na pia kutumiwa na na Simba kwa ajili ya kukashifu mazuri yote ya Yanga.

Ukianzia pale Efm kitengo chao cha michezo wao mwanzo mwisho na kuiponda yanga na kuisifia Simba.

Kwa kuwashauri Yanga imeshatoka huko kufanya mambo kwa kutegemewa kusifiwa na Wachambuzi bila imefocus kwenye mambo makubwa zaidi.

Wanayanga endeleeni kushikama kwa Sana bila kusahau kuwaombea viongozi wenu ulinzi wa Kimungu kwani kuna maadui kila pembe hakuna anayependa mafanikio yenu.
 
Kwahiyo Hersi ndio kamuoa Manara au Manara kamuoa Hersi?

Au wote wameachwa na wake zao?

Au Kabwili kafanyaje?

Utopolo kuna kazi sana...

Hili nalo mkalitazame, au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kwahiyo Hersi ndio kamuoa Manara au Manara kamuoa Hersi?

Au wote wameachwa na wake zao?

Au Kabwili kafanyaje?

Utopolo kuna kazi sana...

Hili nalo mkalitazame, au nasema uongo ndugu zangu?

Ukisoma vizuri mada nimesema baadhi ya Watanzania Wana Roho mbaya, uchawi, fitna, majungu, tamaa mbaya...nk jichagulie mwenyewe hapo una fit wapi.
 
Nishatambua akili zako ila ndio tabia za Wanasimba no hoja matusi ndio nyumbani.
Hongera boss kwa kuwa na kamusi ya matusi na lugha chafu kichwani.

Keep it mwamba
Ahsante sana mkuu ndugu yangu.

Nawe nakuombea upate akili ya kuandika mambo ya maana....
 
Kwahiyo Hersi ndio kamuoa Manara au Manara kamuoa Hersi?

Au wote wameachwa na wake zao?

Au Kabwili kafanyaje?

Utopolo kuna kazi sana...

Hili nalo mkalitazame, au nasema uongo ndugu zangu?
Wewe sio gentleman. Unawaza kawaida sana

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…