Uchaguzi 2020 Wapenda soka wamejipanga kuishikisha adabu CCM kwenye uchaguzi huu

Uchaguzi 2020 Wapenda soka wamejipanga kuishikisha adabu CCM kwenye uchaguzi huu

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Soka ndio mchezo unaopendwa zaidi na watu wengi hapa Tanzania. Mchezo wa soka hauna itikadi, lakini chini ya utawala wa CCM, mchezo wa soka umelazimishwa kuwa wa kiitikadi za kisiasa.

Kwa uchache hizi ni baadhi ya viashiria vya wazi vinavyofanywa na CCM ambavyo vimewakera sana wapenda soka hapa Tanzania.

1. Viwanja vingi vya soka kuwa mali ya CCM. Hii inalazimisha watumiaji wake kuipigia magoti CCM ili kupewa ruhusa ya kuvitumia. Na wakati huu wa kampeni viwanja hivyo vimejazwa bendera na picha za wagombea wa CCM tu.

2. Kuwalazimisha mashabiki wa timu kongwe na kubwa za mpira za Yanga na Simba kuwa sehemu ya wapenzi wa CCM. Hapo awali ilionekana labda timu ya Yanga ndio yenye mwelekeo wa kiitikadi za CCM (kwa sababu ya rangi zake na historia yake) lakini kwa sasa hali imeingia kwa klabu ya Simba pia, ambapo msemaji wake (Haji Manara) na Mmiliki wake (Mo Dewji) wote wameitumia Simba kama jukwaa la kuinadi CCM. Na mwelekeo huo umeanza kuingia pia kwa klabu za Azam, Namungo nk.

3. Uharibifu wa kimakusudi wa uwanja wa Mkapa, uwanja ambao ndio mkubwa na wenye hadhi zaidi kimichezo hapa Tanzania. Uwanja ule ndio kioo cha soka la nchi yetu kimataifa. Kitendo cha kuufanya uwanja(Pitch) kuwa sehemu ya kuweka majukwaa na kurundika watu wakati wa kampeni za CCM juzi kuliuacha uwanja ule kuwa kama jalala la takataka na kuchimbwa chimbwa mashimo madogo madogo mithili ya shamba ya mihogo lililovamiwa na panya wa porini wenye njaa.
 
Haya subiri tarehe 28 Oct ukaishikishe adabu CCM baada ya hapo urudi utupe mrejesho!
 
Back
Top Bottom