Wapenzi wa jinsia moja wapinga sheria hiyo Uganda

Wapenzi wa jinsia moja wapinga sheria hiyo Uganda

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
1394551777271.jpg
1394551800139.jpg

Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja, mawakili na wansiasa wamewasilisha kesi mahakamani nchini Uganda kupinga sheria mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia mojanchini humo.

Wanaharakati hao, wanasema kuwa sheria hiyo inakiuka katiba ya Uganda na kuendeleza ubaguzi na kukandamiza uhuru wa kujieleza.

Sheria hiyo ilitiwa saini na Rais Yoweri Museveni mwezi jana na imelaaniwa vikali na jamii ya kimataifa.

Rais wa Marekani Barack Obama ameitaja sheria hiyo kama hatua ya ukandamizaji kwa waganda na nchi kadhaa tayari zimetishia kuinyima Uganda msaada.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuwa itachukua miezi kadhaa kabla ya kusikilizwa.

source: Mashoga wapinga sheria Uganda - BBC News Swahili
 
Huko ni kutapatapa kwa shetani na mawakala wake kwa Uganda wasipoteze muda wao.Haki gani ya kumharibu binadamu kimwili na kiroho!
 
Back
Top Bottom