SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Enyi wadau wa Kiswahili. Habari zenu? Nawasilisha hapa misemo hii ninayoisikia kwenye radio na tv na kuisoma kwenye magazeti (hata hapa JF) na napata shida kuielewa.
Naanza kuzungumzia moja baada ya nyingine:
1. Ajali Mbaya: Karibu kila siku nasikia na kusoma msemo huu. Huwa najiuliza, je kama kuna ajali mbaya, ipo vilevile ajalinzuri? Ajali zote zinajulikana ni mbaya. Kwa hiyo ukisema 'Kuna ajali mbaya imetokea Msata, hakuna jipya ulilosema kuhusu hiyo ajali. Pengine ungesema 'Ajali kubwa imetokea Msata',ingekuwa bora zaidi. Kwa hiyo neno 'mbaya' kulitumia kuzungumzia ajali kwangu haileti maana. Wewe waonaje?
2.Mafuriko ya Maji: Hii nimeisikia sana juzijuzi kuhusiana na mvua kubwa zinazonyesha huko Indonesia. Mtangazaji alisema hivi: 'Mafuriko makubwa ya maji yameukumba mji wa Djakarta huko Indonesia baada ya mvua kubwa kunyesha'
Mimi najiuliza mtu akitaja mafuriko, si tayari mtu unapata picha ya maji meeengi yanayotiririka? Kwa nini useme tena
mafuriko ya maji? Kwangu hiyo mimi ninaona ni matumizi mabaya ya maneno. Mawazo yako je?
3.Chini ya Mvungu. Hii nimeisikia sana na inanishangaza. Chini ya mvungu ndo wapi tena huko jamani? Mimi najua mvunguni, yaani chini ya kitanda lakini chini ya mvungu mmhh! Nini maoni yako.
4.Msitu wa miti:Niliisikia siku moja hii nikapigwa na bumbuazi! Nikajiuliza: Kwani msitu ni wa nini? Mawe? Majani?
Mimi naona ukishataja msitu hakuna haja ya kuongeza neno 'miti' Umeshakutana nayo? Tupe maoni.
5. Faulo Mbaya:Hii niliisikia kwenye kipindi cha michezo. Mtangazaji alisema: 'Mchezaji wa timu X alimfanyia faulo mbaya mchezaji wa timu Y na refa akaamuru ipigwe penalti' Kwani kuna faulo nzuri? Ebu toa maoni yako.
6.Amekufa kabisa: Nayo hii nimekutana nayo mara kadhaa. Maoni yangu ni kwamba kufa ni kufa hakuna kufa nusu wala kufa kidogo.
Pengine ipo misemo mingi zaidi isiyoleta maana ambayo sijaitaja. Kama waifahamu ee mpenda kiswahili, iweke hapa
Asanteni.