Wapenzi wa NBC Premier League, nini kifanyike tupate ladha halisi ya mpira?

Jamaldini kassimujr

Senior Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
142
Reaction score
101
LICHA YA KUWA NA UDHAMINI MZURI WA BENKI YA NBC NA WADHAMINI WENGINE.

Lakini mbona bado hatuipati radha halisi ya mpira hususa ni kwa hizi timu zetu ambazo tunategemea zifanye mapinduzi

Nini kifanyike wadau ?
 
LICHA YA KUWA NA UDHAMINI MZURI WA BENKI YA NBC NA WADHAMINI WENGINE.

Lakini mbona bado hatuipati radha halisi ya mpira hususa ni kwa hizi timu zetu ambazo tunategemea zifanye mapinduzi

Nini kifanyike wadau ?
Waje wadhamini hata mia kwa viwanja tulivyo navyo tutaendelea kuona pira bisi mpk Dunia inaisha

Viwanja viboreshwe kwanza hakika utaona kandanda safi kutoka Dodoma,Geita Gold,Coastal,Namungo,prison n k
 
Japo utawala wa Jamal Malinzi uliingia doa lakini mkakati wake wa kuhakikisha viwanja vinaboreshwa niliupenda

Alianza na Nyamagana stadium akaweka nyasi bandia, ikafuata Kaitaba stadium ikakamilishwa, ila kabla hajaenda viwanja vngne utawala wake ukala mweleka

Wallace Karia inabidi aendeleze huu mkakati wa kuboresha viwanja maana ubovu wa viwanja unapunguza sana ladha ya mpira mtamu ktk ligi yetu

Kwa hivi sasa tuna viwanja Vitano tu nchi nzima vilivyo ktk ubora mzuri,,, Mkapa, Uhuru, Chamazi, Kaitaba na Nyamagana
 
Kirumba,jamhuri Dodoma na morogoro na vingine vilivyopo ilikuwa na ccm virudishwe kwani vilijengwa kwa kodi za wananchi.

Virudishwe ili serikali ivikarabati na kuweka pitch za kisasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…