Wapenzi Wa Riwaya za Hayati Ben R Mtobwa

Wapenzi Wa Riwaya za Hayati Ben R Mtobwa

Jaya_lchemist

Senior Member
Joined
Oct 12, 2022
Posts
123
Reaction score
207
Nisomapo kazi ya Mtobwa mimi huguswa na jinsi mwandishi huyu alivyocheza na lugha. Naam, anaelezea tukio kwa lugha inayovutia.

Lengo langu ni mtu aliyeguswa na kazi fulani atupie kitabu huku au ataipu sentensi chache zilizomfurahisha. Njia hii itawasaidia waandishi waboreshe uwezo wao wa kulielezea tukio au hisia kwa weledi
 
KAMA maji ya bahari ya hindi yangekuwa na hisia, basi yangejisiskia fahari sana kwa kupata fursa nyingine ya kuiburudisha miili ya viumbe hawa wawili ambao walikuwa wakiogelea kandokando ya ufuko huku wakicheza na kucheka.

Walifanya picha ya kuvutia sana, hasa sura zao nzuri zilipoibuka na kutoka majini na kumezwa na tabasamu lililosababishwa na mzaha waliokuwa wakifanyiana chini ya maji. Baada ya kuogelea kwa muda walirejea nchi kavu ambako walijibwaga juu ya mchanga ulioruhusu joto likaushe maji miilini mwao.

Ufuko pia ungekuwa na kila sababu ya kusherehekea johari ya kulaliwa na viumbe kama hawa kwani walioana kimaumbile kama pacha, ingawa hawakuwa mtu na dada yake.

Walikuwa kama jozi ya kiatu cha kiume kwa cha kike. Mwanamume hakuwa mwingine zaidi ya yule kijana mwenye umbo refu, kakamavu, lililokaa kiriadhariadha na sura nzuri, yenye dalili zote za hekima, ushujaa na ucheshi. Kwa jina anaitwa Joram Kiango.
 
Tupo lakini mistari tumesahau

Nimekumbuka huu hapa “ukimpata muue halafu tutamuuliza maswali baadae “ huyo alikua chongo kwenye dimbwi la damu
 
Vitabu gani hebu tukumbushe maake wengine shule tumetoka miaka ya 90
 
Tutarudi na roho zetu
Dar es salaam usiku
Pesa zako zinanuka
Najisikia kuua tena
Roho ya paka
Zawadi ya ushindi
Mwamba Ben R.Mtobwa alikua gwiji wa hadithi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom