Wapenzi wa rooftops (migahawa na kumbi zilizopo juu ghorofani) njooni hapa

Wapenzi wa rooftops (migahawa na kumbi zilizopo juu ghorofani) njooni hapa

Dharra

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2017
Posts
1,661
Reaction score
2,963
Habari za jioni wakuu.

Nakumbuka wakati nipo Dar nilikuwa mpenzi mkubwa wa kutembelea rooftop bars ama restaurants.

Kila mwezi nilipendelea sana kutembelea aidha Holiday inn roof top, Harbor view roof top, New African Hotel roof top na zingine.

Nilipenda sana mandhari hizi kwa sababu zilikuwa ni tulivu na unapata huduma kwa thamani ya fedha yako. Ingawa baadhi ikifika mida ya night kali zinavamiwa na changudoa na kuharibu/kukoleza taswira halisi ya sehemu husika.

New Africa restaurant walikuwa na chef mahiri sana na msosi wao ulikuwa wa uhakika sana, mwanga hafifu na huduma bomba sana. Taswira ya mwanga unaoangazia bandarini na meli zinazopakuwa mizigo nyakati za jioni zinakupa view moja matata sana.

Harbor view roof top pembeni ya ile swimming pool unaweza kumaliza hata vikombe kumi vya kahawa na ukaendelea tu kutulia, ingawa sometimes panavamiwa na dada poa wa kichina wanaotegesha pale chini Grand casino.

Holiday Inn kila alhamisi roof top kunanoga kwa nachi za kiarabu, na jamaa wa pale bar ni mjuzi sana wa kuchanganya cocktail za kufa mtu ingawa napo sometime panafurika changu.

Wewe ni shabiki wa rooftop gani? Karibuni leta ushuhuda wako.

cc GuDume Mshana Jr , Sky Eclat
 
Aisee, mi nimeishia holiday inn, high spirit na revolving restaurant Akemi kwa huko mjini, masaki na mbezi beach ndio angle zangu, raha sana kumpeleka mshamba mshamba pale Akemi
 
Mkuu kuna Hotel moja Bagamoyo(Jina limenitoka) inarooftop nzuri ,,,Ni Arc flani kwa design na haina madada poa kama Hoteli nyingi za Dar.
 
Huitaji mamilioni,,,,Ukiwekewa hata boom ,,unamega kiduchu na kwenda kuona ToP View Ya Dar,,,,

Kumbuka Mawazo ya Kimasikini ndio kikwazo cha maendeleo,,
 
Mkuu kuna Hotel moja Bagamoyo(Jina limenitoka) inarooftop nzuri ,,,Ni Arc flani kwa design na haina madada poa kama Hoteli nyingi za Dar.
Jaribu kukumbuka mkuu,maana bagamoyo ndo mitaa yangu ya kujidai wikiendi
 
High Spirit
high-spirit-lounge-bar.jpg
 
aisee hao wachina si wanaogopaga dushe nyeusi, hadi uwabembeleze sana
ahahah Mkuu falcon mombasa ukiweka dau la maana mezani hakuna kinachoshindikana. Unjua sehemu hizi bidhaa ni expensive sana kwa hio population huwa ni ndogo mnoo. Kama umezoea nyomi na unaboreka mkiwa kidogo sehem hizi sio za kwenda, wakati mwengine utajikuta masaa mengi upo tu peke yako.
 
Aisee, mi nimeishia holiday inn, high spirit na revolving restaurant Akemi kwa huko mjini, masaki na mbezi beach ndio angle zangu, raha sana kumpeleka mshamba mshamba pale Akemi

Mi mpaka naondoka bongo sehemu hizo ilikuwa bado hazijafunguliwa rasmi, natamani sana siku nikija nitembelee huko. kukoje mkuu?
 
Mkuu kuna Hotel moja Bagamoyo(Jina limenitoka) inarooftop nzuri ,,,Ni Arc flani kwa design na haina madada poa kama Hoteli nyingi za Dar.

Kaka FAIZHAD ningependa kuitembelea hio pia. Anything special hapo?
 
Back
Top Bottom