"Timu ya Twiga Stars IMEWEZA kupata ajali na mchezaji mmoja AMEWEZA kujeruhiwa" - By Isack Gamba.....Kipindi cha JARIDA LA MICHEZO Jumamosi 20/3/2010
Too low.
Mtu mzima hajui jinsi ya kuunda sentensi na matumiza ya maneno. I changed channel hapo hapo baada ya hiyo sentensi
ITV na Radio one wanakosa watangazaji wenye mawazo ya kisasa, wenye uwezo wakubuni vipindi vya micheza katika namna ya kumvutia msikilizaji, kina Gamba, kitenge na Rweyeyunga wamekuta vipindi vya michezo vilivyobunia na kusanifiwa na kina Abdalah Majura, Abuubakary Lyongo, Mikidadi Mahamudu.....wameshindwa kuvitengeneza vikaw vipindi maridadi kwa wasikilizaji wakileo.Ni aibu! Hao ndio wanajidai kususia kutangaza habari za wakali SIMBA! Ni afadhali waendelee kususia milele ili tusahau kabisa kwamba kuna kitu kinaitwa Radio One au ITV.
...Nachelea kusema kuwa yale aliyokuwa akiponda Masanja wa Ze Comedy ndio yanathibitika hapa sasa. Hivi inawezekana vipi mtu mwenye pesa zako na unafanya biashara za uhakika katika media indistry eti mnawekeana bifu na Simba? Uswahili mtupu...Iko siku wenyewe watarudi kundini na watarusha habari za wekundu wa Msimbazi na tutawazodoa tu..!!!Hakuna haja ya kusumbua kichwa kufikiria vyombo vya IPP na coverage ya Simba,after all kuna media nyingi zenye akili kama Star TV ambao nao walifanyiwa vurugu na Simba lakini wakamaintain profession.Tabia za kususa zimezoeleka IPP si unakumbuka waliwahi kuisusa Yanga kisa Manji kuwa mfadhili wa klabu hiyo?Hakuna cha kupoteza IPP waendelee na ukanjanja wao Simba tuendeleze mapambano hakuna wanachoathiri kwetu.