Wapi Maalim Seif kafanana na Mwalimu Nyerere?

Wapi Maalim Seif kafanana na Mwalimu Nyerere?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PLUS TV BURIANI MAALIM: WAPI MAALIM KAFANANA NA MWALIMU?

Leo asubuhi Plus TV walinitembelea nyumbani kunihoji kuhusu vipi Maalim alivyojenga Demokrasia Tanzania.

Kipindi cha saa nzima.

Tunakaribia kuhitimisha kipindi Mtangazaji Jumanne Juma mithili ya chui aliyejificha kichakani akanivamia na swali ambalo hakika sikulitarajia.

Anataka nimpe sifa tano za Maalim zilizofana na sifa tano za Mwalimu.

Swali la papo kwa papo.
Jibu la papo kwa papo.

Tulikuwa tumesimama Maktaba Jumanne anaangalia vitabu vitatu vya historia ya Julius Nyerere.

Nikamchomolea na kitabu cha maisha ya Abdul Sykes bahati mbaya hakuwa anakijua kitabu hiki.

Ameahidi kukisoma ili tufanye kipindi.

20210221_124855.jpg
 
Mzee wangu heshima yako. Lengo hasa la uzi huu ilikua nini?

Tafadhali sana kwa usumbufu wangu kwako.
 
Nimependa ile story ya 7 billion alizopewa na Sultan wa Brunei.
Halafu kuna wehu wanamfananisha Maalimu na Lissu, pamoja na yote Wazanzibar hawana tamaa za utajiri kama hawa wa kwetu wanaojijengea mahekalu kila sehemu hata kama wanayo, kinachonishangaza ni kukinai kimaisha kwa Waislamu wa Zanzibar tofauti na hawa wa bara, Maalimu ameishi maisha ya kawaida sana.

Nakumbuka kuna wakati nilionyeshwa nyumbani kwake kule Mtoni, sikuamini kwa mtu mwenye hadhi yake kuishi maisha yale na hata watoto wake hatuwajuia au kuwasikia kujifanya wadai haki kama hao wa wengine ambao babu ,baba zao ndio wamekula keki ya taifa kiulaini na leo baada ya wazazi wao kuwekwa pembeni wanajifanya watetea wanyonge.

Pamoja na kutopenda umimi wa Maalimu Seif kuwa yeye ndie kila kitu lakini hakuwa na tamaa ya kujilimbikizia mimali na uwizi,angetaka angekuwa bilionea tena si wa hizi pesa zetu bali zile Kimarekani,ndio maana alikuwa anarudisha hela ya masurufu,na pia nakumbuka wakati wa misukosuko akijajijinialikuwa anafikia hoteli ya kawaida sana Star times pale liklikuwa jumba la sinema kama sijakosea, tulikuwa tunajua kama Maalim yupo pale kwa kuona umati wa wafuasi wake wakiwa wamejazana nje ya jengo.

Niseme tu nimesikitika na kifo cha Maalimu, kwani nilitegemea mengi mema kwa upande wa Zanzibar kwa kutilia maanani kwamba raisi Hussein Mwinyi ni mtu muungwana, na mwenye heshima, mwenye utii na alimheshimu Maalimu kama baba yake kwani anamjua fika kwa kuwa Maalimu alikuwa msaidizi mkuu wa baba yake.

RIP Maalim Seif.
 
Back
Top Bottom